Breaking News

RC CHALAMILA AZINDUA NA KUKABIDHI MAGARI YA WAGONJWA DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 16 amezindua magari ya wagonjwa na usimamizi shirikishi wa utoaji wa huduma za afya ngazi ya Mkoa tukio ambalo limefanyika Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila baada ya uzinduzi huo amekabidhi magari hayo kwenye Wilaya zote za Mkoa huo ambapo amesema vyombo hivyo vya usafiri vitasaidia kwa kiasi kikubwa Kuimarisha mfumo wa Rufaa za wagonjwa na hasa usafirishaji wa dharura kwa akina mama wajawazito waliojifungua na watoto wachanga katika Mkoa

Aidha RC Chalamila amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya katika miundombinu ya Afya vifaa tiba na Wataalam wa Afya, ambapo amesema ni ukweli usiopingika kuwa vifo vya uzazi na watoto wachanga vinachangiwa na ucheleweshaji wa aina tatu, ucheleweshaji katika kufanya maamuzi ya kwenda kupata huduma, ucheleweshaji wa kuzifikia huduma/ usafiri wa rufaa za dharula usioimara, ucheleweshaji wa kupata huduma katika kituo cha kutolea huduma za afya

Hivyo upatikanaji wa magari haya unajikita kupunguza ucheleweshaji wa usafiri wa dharura katika kituo cha kutolea huduma.


Naya Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Mohamed Mang'una amesema magari hayo yanakwenda kupunguza kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji wa usafiri wa dharura kufika katika kituo cha kutolea huduma hivyo amemshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuboresha huduma mbalimbali za Afya

Mwisho RC Chalamila amezindua magari 14 na yote yamekabidhiwa katika Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa Jamii



No comments