Breaking News

MAHARAGANDE ACHUKUA FOMU RASMI KUWANIA NAFASI YA KIONGOZI WA CHAMA TAIFA ACT WAZALENDO

Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria na Katibu Idara ya Haki za Binaadamu na Makundi Maalumu Taifa, Ndugu Mbarala Maharagande akikabidhiwa fomu na Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Ndugu Mohammed Massaga kugombea nafasi ya Kiongozi wa Chama Taifa makao makuu ya chama hicho leo Feb 18, 2024 jijini Dar es salaam.

Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria na Katibu Idara ya Haki za Binaadamu na Makundi Maalumu Taifa, Ndugu Mbarala Maharagande akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Kiongozi wa Chama Taifa makao makuu ya chama hicho leo Feb 18, 2024 jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam
Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria na Katibu Idara ya Haki za Binaadamu na Makundi Maalumu Taifa, wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu Mbarala Maharagande leo February 18, 2024 amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Kiongozi wa Chama Taifa makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi fomu na Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Ndugu Mohammed Massaga amesema lengo la kugombea nafasi hii ni kumpokea kijiti kuendeleza kazi nzuri ilianzishwa na kiongozi wa chama Taifa anaemaliza mda wake Zitto Kabwe ya ujenzi wa taasisi yetu pendwa inayokuwa kwa kasi na kukubalika na Watanzania wengi.

"Uamuzi huu nimefanya mara baada ya kutafakari kwa kina, kujipima, kujitathmini na kufikia hitimisho kwa kujiridhisha pasina shaka kuwa nina uzoefu wa uongozi wa kutosha na wakati sahihi ni sasa wa mimi kumpokea kijiti Kiongozi wetu Mwami Zitto Zubeir Kabwe ili kuendeleza kazi nzuri ya ujenzi wa Taasisi kutokana na kuwa na uzoefu wa uongozi wa kutosha, hivyo ninatosha kushika nafasi hii kubwa ya Uongozi ndani ya Chama chetu" Alisema Bw. Maharagande

Alisema kama nikipata ridhaa ya kuongoza chama nitakaa na wataalamu kupanga mikakati mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa chama kinaendelea kuenzi kazi nzuri iliyoanzishwa na kiongozi wa chama Taifa pamoja kuandaa mikakati ya kuhahikisha kuwa chama chetu kinaelekekea kuweka recodi mpya katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, madiwani na wabunge na hata kushika dola.

Maharagande ametaja mikakati hiyo ambayo ataitumia pindi atakapopata ridhaa kuwa kiongozi wa chama kuwa ni pamoja na Kutekeleza kikamilifu majukumu ya kiongozi wa chama Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 83(1) na (2) inaeleza kazi na majukumu ya Kiongozi wa Chama ambayo ni; kuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia; mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji mkuu kwa viongozi wote na maafisa wa Chama, kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu, kuwa mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa Chama katika mambo ya kitaifa na kimataifa; kuwa mtoa habari mahsusi kwenye Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa;
 
Ametaja mengine kuwa ni Kuendeleza mazuri yote ambayo Kiongozi wetu wa Chama anayemaliza muda wake ameyafanya kwa umahiri na juhudi kubwa kukifikisha Chama katika hali ya fahari ambayo kila mmoja wetu hivi sasa anajivunia nayo. Malengo na Madhumuni ya Chama, falsafa na itikadi ya Chama imeelezwa vizuri katika Katiba ya Chama chetu.

Aidha Maharagande ametaja vipaumbele vingine kuwa ni kuwaunganisha Wanachama wote ndani ya Chama ili tuendeleze mapambano yetu dhidi ya CCM, umoja imara uliokuwepo baina ya Viongozi wetu ndio silaha kubwa ya mafanikio ya ukuaji wa kasi unaoridhisha wa Chama chetu. Uwajibikaji ndani ya chama na serikalini  ambapo kila Kiongozi aliyechaguliwa na au kuteuliwa ndani ya Chama anatekeleza majukumu yake ipasavyo na pale anaposhindwa kwa namna moja au nyingine Katibu Mkuu atamsaidia kutatua changamoto zilizopo.

Vingine kuwa ni kuhakikisha kunakuwepo na kushirikiano kati chama Bara na Zanzibar kwa kutumia njia mbalimbali na nashinikiza utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marehemu Maalim Seif (Rahimahullahu Alayhi) na Dk. Hussein Ali Mwinyi, -Rais wa Zanzibar yanatekelezwa kwa vitendo kwa kuwekewa ratiba makhsusi ya utekelezaji.

Alisema katika uongozi wake atahakikisha kuwa anatekeleza Maoni ya wadau juu ya uboreshaji wa mifumo ya kisiasa Zanzibar kama vile hatua zilizochukuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatekelezwa kwa Kushughulikia masuala ya siasa na uchaguzi kwa ujumla wake.

Aidha atahakikisha pia tunaendeleza madai ya kuwa na Muungano wa Haki na Usawa wenye maslahi kwa pande zote mbili pamoja Muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa unatazamwa upya na kufanyiwa marekebisho ili uendane na mahitaji ya wakati wa sasa kwa maslahi ya Wazanzibar wote.

Zoezi la kuchukua fomu na kurejesha kwa kugombea nafasi mbalimbali katika chama hicho lilizindulia rasmi February 14 litafikia tamati February 26 mwaka huu. 

No comments