Breaking News

WAZIRI BITEKO KUFUNGUA KONGAMANO LA WACHIMBAJI WADOGO NA WADAU WA MADINI NA VIWANDA JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa uliofanyika makao makuu ya STAMICO jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini (CTI) bwana Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa DACOREMA bwana Josephat Mkombachepa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam:
Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko anatarajiwa kufungua kongamano la siku mbili liliandaliwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa lengo la kuwakutanisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini litakalofanyika April 5 na 6 katika ukumbi Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano huo jijini Dar es saalam Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema lengokubwa la kuandaa kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wachimbaji wadogo kwa lengo la kujadiliana na kutatua changamoto zinazowakabili.

Amesema katika kongamano hilo  wachimbaji wadogo watapata wasaa wa kukutana na wadau kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wamiliki wa viwanda na Taasisi za kifedha.

“Katika kongamano hilo washiriki wataweza tukikutana na kujadiliana juu ya changamoto wanazokutana nazo wachimbaji wa madini tofauti tofauti na sio wa madini yote.Ambapo siku ya ufunguzi umeanza na wachimbaji wadogo wa madini ya viwandani,” amesema Dkt. Mwasse na kuongeza, 

“Hivyo kesho ni kwa ajili ya wadau hawa watatu, ili kujua changamoto zao, kujua kwa nini tunatumia malighafi za nje, lengo pia ni kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuhakikisha malighafi zetu zinazalishwa kwa tija,”.

Kwamba katika mkutano huo pia umewaalika wadau wengine kama mamlaka za udhibiti kama vile Mmalaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na nyingine.

Kadhalika watakuwepo wanajiolojia ambao wanahusika na upimaji wa kiwango cha upatikanaji wa madini na ubora wake.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wote wadogo wa madini, wenye viwanda vya madini pamoja na wenye viwanda wanaotumia madini hayo wahudhurie kwa wingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Leodegar Tenga amewasisitiza wamiliki wa viwanda ambao ni wanachama wao kuhakikisha wanatumia malighafi za ndani.

“Nisisitize nchi yetu inataka kujenga uchumi wa viwanda, hivyo linalofanyika kesho ni mwendelezo wa hiyo dhana nchini ya kujenga uchumi wa viwanda,” Alisema Bw. Tenga

No comments