Breaking News

KITENGE NA IRENE KALENGA (BABY MAMA) WATAMBULISHWA RASMI KUWA MABALOZI WA HALISIA REAL ESTATE


Mtangazaji Maarufu wa Michezo Maulid Kitenge akiwa na Irene kilenga (Baby mama) katika hafla ya kutambulishwa rasmi kuwa balozi wa Halisia Real Estate hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Kampuni ya uuzaji wa viwanja Halisia real estate Jana tarehe 20 March 2023 wamempa dili nono la  ubalozi Mtangazaji Maarufu wa habari za Michezo nchini Maulid Kitenge pamoja na Irene killenga "baby mama" Tukio lilifanyika katika ofisi za Halisia zilizopo Tegeta kibo complex Jijini Dar es salaam.

Halisia real estate ni kampuni inayojihusisha na uuzaji wa viwanja na maeneo makubwa kwa ajili ya makazi na uwekezaji mbalimbali.

Kampuni ya real estate kwa sasa imejikita  katika ukanda wa njia ya Bagamoyo, sababu za kujikita Bagamoyo ni thamani ya ardhi kwani njia ya Bagamoyo ni ukanda ambao unakua kwa kasi sana kutokana na karibu wake wa bahari ya hindi na miradi mikubwa ya serikali kama vile Bandari kubwa ya Kisasa inayotarajiwa kujengwa zinga ambapo ni mbele ya kerege ni kituo kimoja kufika kiromo.

Halisia amewateua Maulid Kitenge na Irene killenga kuwa mabalozi kwani ni watangazaji wamenyooka katika kazi zao na pia ni watu sahihi katika kutangaza biashara ya halasia. 

Kitenge Akizungumza mbele ya waandishi wa habari amesema "kampuni ya Halisia real estate inamiliki maeneo yote inayouza hawana longo longo, na pia viwanja vizuri, vimepimwa na kuuza hii yote ni kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika ununuaji wa ardhi"

Kwa upande wake Irene killenga (Baby Mama) alisema Bagamoyo ni mji mkongwe na unaokuwa kwani miradi ya serikali ya maeneo ya viwanda vya EPZA (Economical process zones) upo Bagamoyo hivyo wananchi wachangamkie fursa ya kununua viwanja kupitia Halisia real estate kwani imetoa ofa ya pasaka na wateja watakaonunua msimu wa ofa hii watapatiwa Hati bila ya kuchangia gharama yoyote

Miradi ya Halisia real estate ipo mitano nayo ni mapinga Beach plot eneo lipo mita 700 kutoka bahari ya hindi, ukiwa katika eneo unaona bahari, Eneo Lina zaidi ya SQM 78,000 na limegawa katika viwanja vya SQM 700 hadi SQM 4000 na Bei yake ni kama Bure ni Tsh 20,000 kwa SQM.

Mradi wa Amani Beach lipo karibu na bahari pia ni kilomita chache kutokea mradi wa viwanda pamoja na Bandari mpya inayojengwa Bagamoyo, Eneo Lina zaidi ya SQM 50,000 na Bei yake ni tsh 20,000 kwa SQM

Aliongeza kuwa Mradi wa kerege ni miradi miwili na yote imejaa miti mikubwa ya mitiki ambayo iko kerege CCM yenye viwanja kuanzia SQM 400 - 4000SQM Bei yake ni tsh 16,000 kwa SQM Eneo Lina zaidi ya SQM 48,000

Mradi wa vikawe ni mradi mzuri uliyopakana kabisa na shule ya ST MARIA DE MATHIAS, ambapo barabara ya vikawe ndio inawekwa lami hivi karibuni, Barabara hiyo inaunganisha kibaha na mapinga (BAOBAB SCHOOL) Viwanja vyake kuanzia SQM 500 - 4000SQM,Eneo Lina zaidi ya SQM 40,000 Bei yake ni Tsh 14,000 kwa SQM

Mradi wa kilomo Chagga ni eneo lilopo karibu na shule ya Msingi Kilomo ni kilomita moja kutokea barabara kuu ya Bagamoyo, viwanja vyake ni kuanzia SQM 400-4000SQM Eneo Lina Zaidi ya SQM 32,000 Bei yake ni Tsh 12,000 kwa SQM

Mradi wa Kilomo kiwalani ni eneo lilopo kiromo kiwalani, karibu na shule kubwa ya premier international ni kilomita mbili kutokea barabara kuu ya Bagamoyo viwanja vyake ni kuanzia SQM 400-4000SQM Eneo Lina zaidi ya SQM 25,000 Bei yake ni Tsh 12,000 kwa SQM 

Na pia kuna Mradi wa Goba Center ni eneo lililopo mita 1km kutoka Goba center, viwanja vyake kuanzia SQM 1200 Kuendelea na kuna majengo pia Bei ni Tsh 45,000 kwa SQM malipo yake ni 50% na inayobakia inalipwa ndani ya miezi miwili. 

Halisia real estate maeneo yao yote ni mazuri kwa ajili ya makazi na uwekezaji, ufugaji na hata viwanda wanawakaribisha Watanzania wapenda maendeleo, wapate ardhi inayopanda thamani. 

No comments