JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUFANYA UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO NCHI NZIMA
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limezindua kampeni ya ukaguzi wa vyombo vyote vya moto nchini yakiwemo magari, bajaji na pikipiki ili kuhakiki usalama wa vyombo hivyo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, kamishna msaidizi mwandamizi SACP Ramadhani Ng’anzi amesema kampeni hiyo ambayo imeanza rasmi leo Februari 6 hadi machi 13/2023 ambapo kutakuwa na kilele cha wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
"Jampeni hii ya ukaguzi wa vyombo vyote vya moto nchini inaanza leo 6 February na inaendelea hado 13 March ambapo utafanyika ukaguzi wa vyombo vyote ikiwemo Magari, Bajaji pamoja na Pikipiki" alisema SACP Ng'anzi.
Aidha amewataka Makamanda wa mikoa wa vikosi vya usalama barabarani nchi nzima kutenga maeneo maalum ya kufanya ukaguzi huo katika mikoa yao na kuhakikisha kila gari, pikipiki na bajaji zinakaguliwa.
SACP Ng'anzi ameongeza kuwa mara baada ya zoezi la ukaguzi huo kufanyika katika vyombo hivyo vya moto jeshi hilo litabandika stika maalum kwenye vyombo hivyo ambapo kwa gari za biashara watalipa shilingi 7000, gari za kawaida zisizo za biashara (binafsi) shilingi 5000 ambapo pikipiki na bajaji zitachangia shilingi 2000 kama gharama za stika hizo.
Alisema mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha ukaguzi huo na ikibainika kuwepo kwa vyombo vya usafiri ambavyo avikufanyiwa ukaguzi na kupatiwa stika ya ukaguzi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wenye chombo ikiwemo kukamatwa na kuondolewa barabarani.
SACP Ng'anzi alifafanua kuwa kazi ya jeshi hilo ni kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unalindwa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vyombo vya moto vinavyozingatia ubora
No comments