ILALA YAWATAKA WANAWAKE KUKAGUA VITABU NA MABEGI YA SHULE VYA WATOTO WAO
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa akizungumza na Wana wake wa UWT GONGOLAMBOTO katika ziara ya Kamati ya utekelezaji Wilaya ya Ilala
Kaimu Katibu wa Uwt Wilaya ya Ilala Mariam BAKARI akizungumza na Wanawake wa Uwt kata ya Gongolamboto
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake WIlaya ya Ilala Neema Kiusa akikabidhi kadi za Uwt Kwa Mwananchama mpya Kata ya GONGOLAMBOTO
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake WIlaya ya Ilala Neema Kiusa (katikati) akiwapa kiapo wanachama wapya wa uwt Gongolamboto ambapo Kata ya Gongolamboto UWT imevuna wanachama 250
Na Heri Shaaban (Ilala)
Umoja wa wanawake UWT WIlaya ya Ilala imewataka Wanawake wa wilaya ya Ilala kuweka utaratibu wa kukagua vitabu vya shule vya watoto wao Pamoja na mabegi.
Akizungumza na Wanawake wa GONGOLAMBOTO Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Wilaya ya Ilala Neema Kiusa, katika ziara ya Kamati ya Utekekezaji uwt WIlaya ya Ilala .
"Tamko letu Kamati ya utekelezaji Umoja wa wanawake Uwt Wilaya ya Ilala kuwataka wazazi kukagua vitabu vya SHULE pamoja na mabegi ya watoto wao kuna vitabu vinaeneza masuala ya mapenzi ya jinsia Moja sio vizuri kwa Jamii YETU Tanzania " alisema Neema .
Mwenyekiti Neema alisema Dunia kwa sasa imebadirika wazazi tukemee vitendo vya mapenzi ya jinsia Moja tuwe makini kwa watoto Wetu kuzungumza nao kila wakati na sambamba na kukemea vitendo hivyo .
Mwenyekiti Neema alisisitiza kila wakati inatakiwa tukague mabegi ya Watoto hivyo vitabu vina chata sio nzuri ya masuala ya ushoga na bendera vinaelezea mapenzi ya jinsia Moja havina maadili .
Wakati huo huo Umoja wa wanawake Uwt Wilaya ya Ilala imewataka wanawake wa Wilaya ya Ilala kulinda Watoto wao wasipotee kuingia katika vitendo viovu.
Alisema uchungu wa mwana ajuaye mzazi mama ndio mlezi wa familia hivyo mzazi unajukumu kubwa la kulea mtoto asiingie katika Makundi hatarishi Uwt inaeneza Siasa pia kuwalinda watoto
Neema alisema dhumuni la ziara hiyo kamati ya Utekekezaji Uwt Wilaya ya Ilala kuwashukuru Wanachama na kuongeza uhai wa Jumuiya hiyo ambapo Kata ya GONGOLAMBOTO Umoja wa Wanawake imevuna Wanachama 250.
Kaimu Katibu wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Ilala Mariam Bakari aliwataka UWT Kila shina waunde kamati ya watu watano katika mashina ya CCM .
Mariamu aliwasisitiza Wanawake wa Uwt kulipa ada kwa wakati pamoja na kujisajili katika mfumo wa electronic.
No comments