Breaking News

CUF KUZINDUA RASMI MKUTANO YA HADHARA KINONDONI 11 FEB 2023

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Taifa Profesa Ibrahim Lipumba anatarajiwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mikutano ya hadhara katika wilaya ya kinondoni utaofanyika katika viwanja vya magomeni kanisani  siku ya tarehe 11 mwezi huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya kuelekea ufunguzi wa mkutano huo mwenyekiti CUF wilaya ya kinondoni bwana Rajab Salum amesema maandalizi yote kuelekea siku ya mkutano huo mkubwa ikiwemo vibali vya kufanya tukio hilo yamekamilika


"Maandalizi yote ya mkutano tayali yamekamilika nichukue nafasi hii kiwataka wapenzi na wanachama wa chama cha wananchi CUF wilaya ya kinondoni pamoja ma maeneo jirani kujitokeza kwa wingi siku hiyo 11 February 2023 ". Alisema bw. Salum.

Aidha bwana Salum alibainisha kuwa mgeni rasmi ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba amedhibitisha uwepo wake siku hiyo ametoa wito kwa wapenzi, wafuasi na wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuanzia sa 8 mchana.

Pia mwenyekiti huyo aliongeza kuwa siku hiyo ya ufunguzi kutakuwepo na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa mziki wa kizazi kipya pamoja na wasanii wengine.
Kwa upande wake mmoja wa wasanii ambao wanatarajiwa kutumbuiza siku hiyo ya ufunguzi bwana Amigo amesema amejindaa vizuri kuhakikisha anatoa show kali siku hiyo ili kuburudisha wapenzi na washabiki wake. 

"Niwatake mashabiki wnagu na wapenzi wa chama cha wananchi CUF kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 11 February pale katika viwanja vya kanisani-Moroco kwani nimejipanga kufanya show moja kali kabisa ambapo pia wanachama hao watapata wasaa wa kusikiliza sera bora za chama makini kutoka kwa Profesa Lipumba"

No comments