Breaking News

PROPHET PHILBERT PASCHAL: 2023 NI MWAKA WA BARAKA, AHIMIZA UPENDO, USHIRIKIANO

Nabii na Mtume wa Kanisa la Bwana Yesu kwa Mataifa Yote lililopo Tabata Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Philbert Paschal amewataka Watanzania kupendana na kishirikana na Serikali ili kuhakikisha Tanzania inasonga mbele.

Akuzungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa mtandao huu yaliyofanyika Desemba 30, 2022 kwa lengo la kutoa neno la mwaka mpya kwa Watanzania kwa mwaka mpya wa 2023.

Alisema mwaka 2023 utakuwa wa heri na baraka kwa Watanzania na kwamba uchimu wa Tanzania utazidi kukua na kuimarika.

“Tumshukuru Mungu Watanzania tuko salama na tuna uzima. Kwa mwaka 2023 Mungu ataisaidia Serikali, uchumi wa Tanzania utazidi kukua, na Serikali itafanya mambo makubwa,” alisema Nabii Paschal wa Kanisa la Bwana Yesu kwa Mataifa Yote na kuongeza,

“Utakuwa ni mwaka wa baraka, Wafanyabiashara watafanya viziri, Viongozi watafanya vizuri na na Watanzania wote watabarikiwa,”.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri katika utumishi wa kuwatumikia Watanzania kwa mwaka 2022.

Hivyo aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuhakikisha afya za wananchi zinakuwa salama.

Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili, alisema kwama vinafanyika kwa sababu ya ukosefu wa maarifa, hivyo watumishi wa Mungu wanapaswa kuwapa waumini maarifa juu ya vitendo hivyo ili viweze kukemeshwa.

Kuhusu mipango ya kanisa kwa mwaka 2023, Nabii Paschal alieleza kwamba wamejipanga kuhudumia Watanzania kiroho na kimwili.

“Vile vile tutashirikiana na Serikali kuhakikisha usalama na amani kwa Watanzania vinaendelea kudumu,” alesema Nabii Paschal.

Kwamba kupitia taasisi ya Prophet Philbert Foundation wamejipanga kuwahudumia wahitaji kwamba wanatarajia kuifikia jamii kubwa ya Watanzania.

No comments