Breaking News

CUF WALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA ULINZI MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA

Chama cha Wananchi(CUF) kimelitaka jeshi la Polisi nchini kutoa ulinzi wa mikutano ya mbalimbali ya kisiasa iliyotangaza kurusiwa na Rais Samia suluhu Hassani.

Pia chama hicho kimeahidi kuwa kitafanya siasa za kistaarabu na zenye tija kwa lengo la kujenga chama cha CUF .

Hayo yameelezwa leo na ijini Dar es Salaam na  Naibu Mkurugunzi wa mipango na Uchaguzi wa  (CUF) Yusufu Mbungiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia kuruhusiwa mikutano ya hadhara wa kwanza chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho kata ya Manzese wilaya ya Ubungo jijini hapa.

Mungilo, amesema Jeshi la polisi linawajibu wa kulinda raia na mali zake hivyo chama hicho kinaliomba jeshi hilo kuzingatia sheria katika kuilinda mikutano kwa kuhakikisha kunakuwa na usalama na Amani.

Hata hivyo Mungilo, amesema chama hicho kinampongeza Rais Samia kwa hatua yake ya kuruhusu mikutano ya hadhara kwa kusema kiongozi huyo ameonesha ukomavu wa hali ya juu kwa kuvifungulia vyama vya siasa vilivyofungiwa takribani miaka sita.

No comments