Breaking News

NABII DKT. KIMANZA VIJANA FANYENI KAZI BADALA YA KULELEWA..KAZI ULINDA HESHIMA YA NDOA

Mtume na Nabii wa Kanisa la Jesus of Power Miracle Church ambaye pia ni Askofu Mkuu Dkt. Joachim Kimanza akihubii katika ibada ya kuaga mwaka 2023 na kukaribisha mwaka 2023
Mtume na Nabii wa Kanisa la Jesus of Power Miracle Church ambaye pia ni Askofu Mkuu Dkt. Joachim Kimanza akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari katika ibada ya mkesha kuaga mwaka mpya na kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Dar es salaam:
Mtume na Nabii wa Kanisa la Jesus of Power Miracle Church ambaye pia ni Askofu Mkuu Dkt. Joachim Kimanza amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii lili kuhudumia jamii badala ya kusubiri kulelewa na akina mama wajane na watu wazima wenye mali.

Akofu Dkt. Kimanza alibainisha hayo akizungumza na waandishi wa habari katika usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya wa 2023 uliofanyika katika Kanisa hilo lililopo Kata ya Saranga, Halmashauri ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam.

Askofu Dkt. Kimanza kufanya kazi ni jambo jema kwani pasipo kufanya kazi familia zinakaa kwenye aibu, uchumi wa nchi unashuka, watu wanapoteza heshima za ndoa na familia, hivyo aliwakaribisha watanzania kainisani kwake kwa ajili ya kuwapatia maarifa ya ujasiriamali na uchumi.

“Na mimi nimekuwa nikiwajenga watu kwa ajili ya kufanya kazi ili wapate kitu cha kubariki kwa sababu tukipofanya kazi maana yake ni kwamba kazi za mikono Mungu anazibariki mtu asipofanya kazi Mungu hana mahali pa kubariki. Ili tuliongezee nguvu Taifa ni lazima tuwe na ibada kwa ufupi lakini muda mwingi tuutumie kwanye kazi,” alisema Askofu Kimanza na kuongeza,

“Hivyo na waasa Misikitini, Makanisani na sehemu zingine zozote watu tufanye, hilo ndilo jambo jema, pasipo kufanya kazi familia zinakaa kwenye aibu, uchumi wa nchi unashuka, pasipo kufanya kazi tunapoteza heshima za ndoa na familia, hili ni jambo la msingi sana. Ili uwe mwanandoa mwema ni lazima uonekane umemeba majukumu yako,”.

Alisema “Lakini mtu ukiona leo imefikia mahali vijana umri mdogo wanatafuta wamama wajane ambao wameachiwa mali zao, wanaenda kujiweka pale wanakuwa marioo hiyo ni aibu sana. Tuanataka vijana wafanye kazi, wahudumie jamii. Nasema vijana ndiyo wenye nguvu ,”

Akizungumzia kuhusu mwaka mpya wa 2023 alisema kwamba umekuwa ni mwaka wenye neema na baraka kwani kwa sababu kuna watu ambao hawakufanikiwa kuuona.

"Leo ni siku ya mwaka mpya 2023, umekuwa ni mwaka wa neema, mwaka wa baraka kwa sababu, kuna watu ambao hawakufika, sasa sisi muujiza wa kwanza ambao tunauona kama Mungu ameufanya ni kuhakikisha sisi tunafika tukiwa salama na wazima na katika utawala mpya wa kitaifa," alisema Askofu Dkt. Kimanza.

Kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimtaka kama kiongoni wa muhimu katika maisha ya Watanzania, kwamba amekuwa ni baraka kwa namna ya ajabu kanamna ambavyo amekuwa akilipigania Taifa kwa huruma na upendo kwa wananchi wake.

Alisema kama Kanisa wamekuwa wakiliweka Taifa mbele za Mungu katika maombi na kuwaombea viongozi kuanzia ngazi ya juu hadi chini yaani kuanzia Rais Dkt. Samia, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mawziri na viongozi wote hadi ngazi ya chini ya Serikali za Mitaa.

Askofu Dkt. Kimanza alitumia fursa hiyo kuyaomba Makanisa na Misikiti inapofikia wakati wa Taifa kwenda kwenye vinyang’anyiro vya uchaguzi kuwe na ulazima wa viongozi walioko madarakani na wasio madarakani, kuwaweka wote mbele za Mungu kwa ajili ya kulinda na kuimarisha amani.

“Lwngo ni kwamba anayeshinda ashinde katika ushindani, ili pawe na amani kwa anayeshinda, na anayeshindwa pia awe na amani, tukubali matokeo na maisha yasonge mbele kwa sababu pasipo amani kwa Taifa, hatuwezi kuabudu, pasipo amani kwa Taifa hatuwezi kusomesha watoto, hatuwezi kwenda mahospitalini, hata mtu aliyepata ajali hawezi kupata matibabu mahospitalini,” alibainisha Askofu Dkt. Kimanza.

Kuhusu huduma ya Kanisa la Jesus of Power Miracle Church Askofu Dkt. Kimanza alisema wamekuwa wakipokea watu wa ndani na kutoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuhudumiwa na kuponywa.

Kwamba kwa huduma hizo kwa hapa nchini wamekuwa wakisaidia wakipunguza msongamano wa wagonjwa mahospitalini, kwa waganga wa kienyeji, na kuwafundisha watu kuhu utaua na kuwapa maarifa ya kumcha Mungu.

“Lakini pia kulifanya Taifa kuwa la amani kwani haliwazi kuwa na amani bila kuwepo kwa kanisa na msikiti,” aliongeza Askofu. Dkt. Kimanza.

Pia wamekuwa kwa sasa wakifundisha mafundisho yenye weledi badala ya kubakia kushikilia mafundisho ya miujiza pekee.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakiwa katika ibada ya mkesha wa kukaribisha mwaka mpya wa 2023 uliofanyika katika Kanisa la Jesus of Power Miracle Church lililopo Kata ya Saranga, wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam.
 

No comments