MAJAMBAZI WALIOVAMIA DUKA GOBA WAKAMATWA
Jeshi la pilisi kanda maalum ya Dar es salaam linashikilia watuhumiwa wa ujambazi sugu wanne wakiwemo Athuman Mbaliko @soti (50) Mkazi wa Kimara Temboni, Mpoki Raphael @mwangisya (41) mkazi wa Mbezi Luis na wengine wawili kwa tuhuma nzito za kujihusisha na vitendo vya unyang'anyi kwa kutumia silaha na kupora fedha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa waliweza kuwaonyesha askari bunduki aina ya AK 27 yenye namba za usajili UCI 3889 1998 ikiwa na risasi 24 ndani ya magazini, bastola moja aina ya Star iliyofutwa namba ikiwa na risasi 4 ndani ya magazine pamoja na pikipiki 2 aina ya boxer nyeusi MC 665 DMD na MC 475 DPH ambazo zimekuwa zikitumiwa kwenda na kutoka kwenye maeneo waliyopanga kufanya uhalifu wao.
Baada ya mahojiano ya kipolisi watuhumiwa hao walikiri kuhusika katika jaribio la uporaji eneo la mtaa wa Tandamti Kariakoo, Uporaji wa pesa huku wakitishia silaha eneo la Mtongani Kunduchi, Goba walitishia silaha na kupora pesa na Keko pamoja na Vikindu iliyopo Mkuranga.
No comments