Breaking News

DKT. MABULA AWATAKA MAOFISA ARDHI KUPITIA MIKATABA YA ARDHI

Na Timothy Marko, Dar es Salaam
Serikali imewataka maafisa wa Ardhi pamoja na watendaji wa Wizara ya Ardhi kupitia kwa upya Mikataba ya Ardhi kisheria.

Akizungumza katika kikao Cha watendaji wa Wizara ya Ardhi jijini Dar es Salaam Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Dokta Angela Mabula amesema kuwa Amewataka Wananchi kushiriki kikamilifu katika  Urasmishaji wa Ardhi kikamilifu.

"Wakurugenzi wa Halimashauri wawe wasimamizi wa Rasmalifedha za wananchi". Alisema Waiziri Mabula.

Aidha, Waziri Mabula amesisitiza maafisa Ardhi na serikali za mitaa kuhakikisha watumiaji wa Ardhi wanaendeleza Ardhi.

Alisema kumekupo na malaloko ya kutoendelezwa kwa Ardhi hususani katika Maeneo ya kigamboni ambapo Mimliki wa Eneo Hilo ni Mfuko wa Hifadhi ya jamii (NSSF) hivyo Amewataka maafisa Ardhi kumsisitiza mmiliki huyo kuliendeleza Eneo Hilo.

"Maeneo yote ambayo hayajulikani Matumizi yake leteni Mapendekezo tuone namna ya kuyaendeleza". Aliongeza Waziri Mabula.
 
Dk Angela Mabula amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa maeneo yote ambayo bado hayajaainishwa kwenye mipango miji yainishwe wazi kwenye Master plan.

"Katikati Nyumba za watu kusiwepo petrol station haiwezekani, Maeneo yaliyovamiwa lazima yazingatie tamko lakiserikali" Alisema Waziri Mabula.

Awali akimkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maakazi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dokta Alan kijazi amesema kuwa zoezi la Urasimishaji ni takwa la kisheria ni kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1995.

Alisema jiji laDar es Salaam linaongoza kuwa na Makaazi ambayo hayarasimishwa.

"Tutaanza zoezi viwanja vilivyomilikishwa muda mrefu huku vikiwa pori, katika hili tutashirikiana na Serikali za mtaa". Alisema Dkt. kijazi.
 

No comments