WANANCHI JITOKEZENI KUPIMA NA KUFANYIWA UCHUNGUZI KAMBI YA MATIBABU HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dokta Rashid Mfaume akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya siku nne ya upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali iliyaondaliwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Dokta Julieth Magandi akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa kambi ya siku nne ya upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali iliyaondaliwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Mwananyamala Dkt. Ilene Balongo akiongea wakati wa ufunguzi wa kambi ya siku nne ya upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali iliyaondaliwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Dar es salaam:
Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kambi ya upimaji na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dokta Rashid Mfaume wakati wa uzinduzi wa kambi ya siku nne upimaji magonjwa mbalimbali iliyoandaliwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Alisema kambi hiyo ambayo imesheheni madaktari bingwa wa magonjwa ya mbalimbali wakiwemo wa mifupa, sukari, moyo, mfumo wa mkojo, macho katika kipundi chote cha kambi hiyo wakitatoa huduma mbalimbali za afya.
“Kambi hii ya siku nne imeandaliwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kwa kushirikiana na Hospitali za Rufaa za mikoa kutoa huduma kwa wananchi haijawahi hivyo napenda kutoa rai kwa wananchi kujitokea kwa wingi kwani kwa kufanya hivyo pia inaongeza umoja na ushirikiano,”. Alosema Dkt. Mfaume
Dkt. Mfaume alongeza kuwa hii ni fursa kubwa wananchi wa wikaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kuchangamka na kujitokeza kwa wingi kuja kucheki afya zao kwa gharama nafuu kabisa.
Aidha Dkt. Mfaume ameeleza kuwa kambi hiyo pamoja na kutoa huduma za kupima na kutoa matibabu pia inatumika kuwajengea uwezo watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Mwananyamala.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Dokta. Julieth Magandi ameushukuru uongozi wa hospitali ya Mwananyamala kwa utayari wao wa kuwa na kambi hiyo.
Alisema hawataishia hapo tu bali wataandaa kambi nyingine zitafanyika katika hospitali mbalimbali ambazo ni pamoja na Tumbi ambapo kambi itafanyika kuanzia Januari 20 hadi 24 mwaka huu.
Amezitaja kambi nyingine kuwa ni katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke itafanyika Machi 6 hadi 10 mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Wizara ya Afya ya kusogeza huduma kwa wananchi.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Mwananyamala Dkt. Ilene Balongo amesema hadi kufikia leo 10 january kambi hiyo iliyoanza jana Januari 9, 2023 imeshahudumia wananchi zaidi ya 260 na mpango ni kuhudumia wananchi 300 kwa siku.
"Mwitiko wa wananchi kuja kuoata huduma sio mbaya japo tunawakaribisha kuja kwa wingi zaidi kwani kwa siku moja january 9 -10 tumeweza kuhudumia zaidi ya wananchi 260 nichukue nafasi hiu kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupatiwa huduma" Alisema Dkt. Balongo.
Wananchi wakipatiwa huduma mbalimbali za matibabu ushauri katika kambi ya siku nne ya upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali iliyaondaliwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mloganzila) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala
No comments