NDC YAANZA ZOEZI LA UNYUNYIZIA DAWA ZA KUULIA VIWADUDU KATIKA MITARO
Halmashauri nchini zimetakiwa kuongeza kasi ya kununa Dawa za kuua viwadudu kwa ajili ya kumaliza mazalia ya Mbu na kuweza kutokomeza ugonjwa wa Malaria.
Rai hyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Rasilimari watu wa Shirika la maendeleo la Taifa (NDC), bwana Harson Jackson, wakati zoezi la umwagiliaji dawa za viwadudu katika mitaa na madimbwi ndani yaKata ya Mabibo mtaa wa Relini Jijini Dar es Saalam ikiwa ni sehemu ya shirika ilo kurudisha kwa jamii.
Aidha, Jackson amesema licha halmashauri kuhimizwa na viongozi wa serikali kununua dawa kuuwa viwadudu lakini bado kasi hailizishi katika kununua dawa hizo na kuzitaka halmashauri kuongeza kasi katika manunuzi ya dawa hizo ili kuweza kuushinda ugonjwa wa Maralia.
Kwa Upande wake Mtaalamu wa Viwadudu kutoka Kiwanda cha viwadudu cha Baotic Product kilichopi mkoani Pwani John Tusiwe, amesema kiwanda hicho kinazalisha dawa za kisasa na bora kwa ajili kuuwa mazalia ya mbu ambazo zitasaidia kuondokana na ugonjwa wa maralia na magonjwa yatokanayo na mbu.
Afisa Uhusiano wa shirika la maendeleo Taifa (NDC),Amina Sanga,amezitaka Taasisi na watu binafsi kujitokeza katika kununua Dawa za kuua mazalia ya Mbu na akisema shirika ilo limejipanga kutoa elimu sehemu mbalimbali nchini juu ya umuhimu wa dawa hizo huku Wananchi wa kata ya mabibo wakiipongeza hatua ya NDC kumwaga dawa na kutaka zoezi hilo liwe endelevu.
Zoezi hilo la umwagaji wa dawa za kuulia viwadudu katika mitaro na madimbeib ambalo ni endelevu nchini limeanza katika kata ya Mabibo manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.
No comments