TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUHAKIKISHA TUNATOA HUDUMA BORA ZA AFYA
Serikali imepongezwa kwa hatua ambazo imekuwa ikizichukua hasa katika kuhakikisha kila mtqnzania anakuwa na bima ya afya pamoja na kuweka mazingira ya kuwashirikisha wadau wa sekta ya afya katika kukamilisha hazma hiyo.
Akizungumza katika mahojiano na mtandao huu jijini dar es salaam Tabibu Emmanuel Tabibu Emmanuel Maduhu Amesema serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wanancho wote wanakuwa na bima ya afya pamoja na kuwashirikisha wadau wengine katika sekta hiyo wakiwemo tiba mbadala.
"Serikali imeonyesha dhimira ya dhati ya kuhakikisha kuwa kila mtanzania anakuwa na bima ya jambo ambalo litasaidia kuwa na taifa bora na lenye wananchi walio na afya bora" Alisema tabibu Tabibu Maduhu
Alisema wao kama wadau muhimu katika kuhakikisha lengo ilo linafaniliwa wamekuwa wakitoa mchango wao kwa serikali kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila mtanzania kwa nafasi yake anapata huduma bora za afya.
Akitolea mfano janga la corona katika kipindi cha rais magufuli alionyesha uzalendo wa dhati kwa hatua ambazo alikuwa akichukua katika kipindi chote cha ugonjwa huo nchini kwa kuwaagiza wananchi kutumia tiba mbadala kuweze kujikinga na janga hilo na matokeo yake wote tuliona.
No comments