ACT WAZALENDO YATAJA MAFANIKIO KAMATI YA KUISIMAMIA SERIKALI YA WASEMAJI WA KISEKTA
Chama cha ACT Wazalendo kimetaja mafanikio kiliyopatikana tangu kuundwa baraza kivuli la mawaziri na Kamati za Kuisimamia Serikali yaani wasemaji wa Kisekta Katika kipndi cha miezi 10 tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kivuli Bi Doroth Semu amesema katika kipindi cha miezi 10 cha utendaji wa baraza hilo kivuli umekuwa na tija kubwa kwani wamefanikiwa kutoa jumla ya matamko rasmi ya kiuchambuzi yapatayo 95 na Mkutano na Waandishi wa habari 31 sambamba na ziara za wasemaji wa kisekta (Mawaziri Vivuli) saba.
Alisema kupitia baraza hilo kivuli wamekuwa wakitoa matamko na chambuzi mbalimbali ikiwemo ya kupanda kwa gharama za maisha kutokana na bidhaa muhimu kupanda bei pamoja na kutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto ili kuleta unafuu kwa wananchi.
Akitolea mfano baadhi ya mapendekezo hayo kuwa ni pamoja na pendekezo la kupunguza au kuondoa kabisa tozo, ushuru na kodi kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ambazo ni muhimu kwa maisha ya watu kama vile mafuta ya kula, sukari, ngano na mafuta ya petroli na diseli.
Ametaja mengine kuwa ni kuongeza uzalishaji wa vyakula na mahitaji muhimu kwa nchi na kuhitaka Serikali kuongeza umakini katika udhibiti wa soko holela la nje (usafirishaji wa chakula nje) kwa lengo la kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu hasa chakula.
“Licha ya Serikali kutekeleza baadhi ya mapendekezo tuliyowahi kutoa japo sio kwa ufanisi na kwa usahihi kama vile ilitoa ruzuku ya mafuta na mbolea, kuondoa kodi kwenye mafuta ya kula na kupunguza tozo za miamala ya kieletroniki (Simu na Benki),” Alisema Bi Semu.
Alisema mwenendo wa mfumuko wa bei nchini (gharama za maisha) bado unazidi kupaa, nitoe rai kwa Serikali kuweka mikakati ya kuhami maisha ya watu na kujiandaa kukabiliana na hali hiyo na kuwaandaa wananchi kuongeza uzalishaji na angalau kukidhi mahitaji ya ndani.
Akizungumzia juu ya Miswada ya Sheria na kanuni iliyopekwa Bungeni, amesema kupitia Kamati ya Wasemaji wa kisekta walifuatilia, kuchambua, kukosoa na kutoa mapendekezo kuhusu miswada kadhaa iliyowasilishwa.
Akitolea mfano Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao uliwasilishwa na Serikali kwa mara ya kwanza bungeni Septemba 2022 pamoja na nia njema ya Serikali ya kutaka kupanua wigo wa watu walio sekta isiyo rasmi kuingizwa kwenye mifumo ya bima, maudhui ya muswada huo yalikuwa na mapungufu mengi.
“pamoja na nia nzuri ya serikali kutaka kilaa.mtanzania kuwa na pima ya afya ila tuligundua tatizo tuliloliona wananchi walio sekta isiyo rasmi wasingeweza kumudu gharama za bima hiyo kutokana na viwango vya juu vilivyowekwa. Pia kiuchambuzi na uhalisia muswada ulikuwa unaimarisha na kukuza madaraja ya kupata huduma bora kama ilivyo sasa, kwa wasio na uwezo na wenye uwezo,” Alisema Bi. Semu
Alisema mifumo ya uchangiaji kutokuwa na uhakika na endelevu, uliwekeza kwenye kutumia mabavu kwa kuzuia watu kupata huduma zingine kama njia ya kuwavutia wananchi kujiunga na Bima ya Afya.
Amesema, waliupinga Muswada huo kwa sababu ulikuwa hauendi kuondoa matatizo ya msingi kwenye upatikanaji wa huduma bora za afya kwa usawa na kwa uhakika hatimaye Muswada uliondolewa rasmi Bungeni, tunatumai sasa kama wadau tutasikilizana ili kuboresha zaidi.
Akizungumzia kuhusu Kuhusu Kanuni ya Kikotoo cha Mafao ya Uzeeni, amesema Serikali ilirejesha kanuni hiyo iliyopigiwa kelele mwaka 2019 na kuifanyia marekebisho madogo.
“Kiukweli, ACT Wazalendo tulipambana kuhakikisha kanuni hizo zisipitishwe na Bunge kwa kutoa mapendekezo mbadala kupitia Kamati hii ya wasemaji wa kisekta,” aAlisema Bi. Semu.
Aliongezaa kuwa uamuzi wa Serikali kutangaza Kanuni mpya uliweka kikotoo cha 1/580 badala ya 1540, pia malipo ya mkupuo ya mafao (kiinua mgongo) ya mtumishi aliyestaafu atalipwa kwa asilimia 33 badala ya 50% iliyokuwa inatumika kabla, umri wa kuhudumiwa mstaafu ni miaka 12.5 badala ya miaka 15.5.
Akizungumzia Kuhusu Muswada wa huduma za Habari amesema waliungana na wanahabari kupaza sauti kuhakikisha muswada huu unarekebishwa kwamba kazi hiyo wataendelea nayo mwaka 2023.
No comments