CUF YATOA TATHIMINI YA HALI YA KISIASA NA KICHUMI KWA MWAKA 2021/22
Chama Cha Wananchi CUF kimetoa tathimini yaliyojili kwa mwaka 2021 na matarajio yetu kwa mwaka 2022 na kutoa Mapendekezo katika maeneo mbalimbali juu ya hali ya Kisiasa, Uchumi, Utawala Bora unaozingatia Sheria na Haki za Binadamu kwa Ujumla wake.
Akizungumza makao makuu ya chama hicho buguruno jijini Dar es salaam mwenyekiti wa CUF taifa Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama kimekuwa na utaratibu wa kuangazia masuala muhimu yanayohusu mustakbali wa taifa letu, kufanya Tathmini ya kufunga mwaka 2022 sambamba na kubainisha matarajio na mapendekezo yetu kwa mwaka Mpya wa 2023, panapo majaaliwa.
"Kama ilivyo desturi ya chama cheti kila mwisho wa mwaka kimekuwa na utaratibu wa kuzungumzia mambo muhimu yanayohusu mustakbali wa taifa letu pamoja na kutoa tathimini, matarajio pamoja na mapendekezo kwa mustakabali wa Taifa" Alisema Prof Lipumba.
Alisema tathimini hiyo itagusia nyanja mbalimbali kiwemo utawala bora unaozingatia sheria, Hali ya kisiasa nchini na kidemokrasia, Jitihada za kufufua uchumi na kukamilisha miradi ya maendeleo pamoja na Ustawi wa wananchi na hali ya furaha kwa mwaka 2022.
Profesa lipumba alisema katika kuhakikisha yote yanatekelezeka kwanza Tunatoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutembea kwenye Hotuba yake ya Kwanza aliyoitoa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hotuba iliyobeba matumaini makubwa kwa watanzania wengi.
Alisema pamoja na mambo mengine hotuba hiyo ilitoa msisitizo juu ya kuachiwa huru kwa wote waliokuwa wakishikiliwa magerezani kwa Kesi za kisiasa na Kesi mbalimbali za kubambikiza, ikiwa ni miezi michache baada ya kilio chetu cha miaka kadhaa juu ya kuwapigania masheikh wa Uamsho kusikika.
Tulitoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutembea kwenye Hotuba yake ya Kwanza aliyoitoa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hotuba iliyobeba matumaini makubwa kwa watanzania wengi.
Alisema hotuba hiyo iligusia mambo mengi ikiwemo msisitizo juu ya kuachiwa huru kwa wote waliokuwa wakishikiliwa magerezani kwa Kesi za kisiasa na Kesi mbalimbali za kubambikiza, ikiwa ni miezi michache baada ya kilio chetu cha miaka kadhaa juu ya kuwapigania masheikh wa Uamsho kusikika.
Sambamba hotuba hiyo pia chama cha wanachi CUF kinamtaka rais Samia kuzingatia pia ajenda ya Maridhiano ya Kisiasa na matarajio yetu ya kushuhudia Mchakato wa kupata Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha Chaguzi zijazo, kuanzia Uchaguzi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji wa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, zinasimamiwa na Tume huru ya Uchaguzi na zinafanyika kwa uhuru na kwa haki.
Akiongelea kuhusu hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini katika kipindi cha mwaka 2022 Profesa lipumba amesema kumekuwepo na matukio ya viongozi wa kisiasa kubbikiwa kesho na kufungwa gerezani akitolea mfano Mhe. Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema), Viongozi na wanachama wa CUF huko Liwale na Lindi, na wananchi mbalimbali.
UTAWALA BORA UNAOZINGATIA SHERIA: Watanzania waliuanza mwaka 2022 wakiwa na mengi mabaya ya kukumbuka. Watanzania kutekwa na watu wasiojulikana, maiti kukutwa zikielea baharini kwenye viroba, watuhumiwa kuteswa kinyume cha Sheria na wengine kufia mikononi mwa Polisi, Wananchi kusota mahabusu muda mrefu kwa Kesi za kubambikiza (zingine zikiwa na masharti magumu ya dhamana) yalikuwa ni mambo ya kawaida kwa Watanzania. Watanzania wengi waliishi kwa hofu na kukata tamaa.
Mwaka 2022 umeshuhudia Kesi nyingi zikifutwa na watu kuachiwa huru; matukio ya watu wasiojulikana hayasikiki tena; Polisi wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa kushiriki jinai dhidi ya wananchi na kubwa zaidi, ni kufumuliwa kwa Safu ya Juu ya Uongozi wa Jeshi la Polisi nchini.
Tunaamini kwamba lengo la Mabadiliko haya katika Jeshi la Polisi na kuundwa kwa Kamati ya Tathmini ya Utendaji wa Jeshi hilo, pamoja na Kikao Kazi cha Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi na Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi kilichoongozwa na Rais Agosti 30, 2022 huko Moshi, Kilimanjaro ni katika dhamira ya kurudisha Amani na kuondoa hofu kwa Wananchi juu ya Usalama wao na wa mali zao.
Watanzania wengi wametega masikio yao kufuatilia kitakachojiri kwenye Uchunguzi wa kifo cha marehemu Stella Moses aliyefia kwenye Kituo cha Polisi Mburahati Desemba 20, 2020, kufuatia Mahakama ya Kinondoni kuamuru hivi karibuni juu ya kufanyika Uchunguzi juu ya kifo hicho.
Chama Cha Wananchi kinatoa Pongezi za dhati kwa hizi jitihada zinazoashiria uwepo wa dhamira ya kuurejesha Utawala Bora na kuhakikisha watanzania wanaishi kwa kujiamini ndani ya nchi yao. Hata hivyo, bado jitihada zaidi zinahitajika katika eneo hili.
HALI YA KISIASA NA DEMOKRASIA NCHINI MWAKA 2022 alisema mnamo 26 Desemba 2021 nilizungumza na Waandishi wa Habari kujadili Maendeleo ya Demokrasia nchini Tanzania uliofanyika tarehe 15-17 Desemba 2021 jijini Dodoma na kueleza kuhusu kongamano hili ilikuwa hotuba ya ufunguzi ya Rais Samia Suluhu Hassan Katika hotuba hiyo kauli iliyonivutia sana ni pale alipoeleza kuwa “hii ni nchi yetu sote hakuna mwenye hati miliki ya nchi hii.” Alisisitiza Vyama vya Siasa vifanye siasa za kistaarabu za kujenga hoja na kueleza sera mbadala na siyo “siasa za chuki, uhasama, na zinazokwamisha maendeleo ya wananchi.”
Alisema Rais Samia alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Vyama vya Siasa kukaa na kujadiliana katika Mkutano huo namna bora ya kufanya shughuli zao za mikutano ya kisiasa bila kuvunja sheria za nchini.
Aidha Mkutano ulifikia muafaka katika mambo muhimu ya msingi, baadhi yake ikiwa ni pamoja na Vyombo vya dola vitende haki kwa sababu haki ndiyo msingi wa amani endelevuSerikali, Vyama vya siasa na wadau wote waheshimu Katiba, Sheria na Kanuni Mchakato wa kupata katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi ukamilishwe ili kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa huru, wa haki na wa amani Tanzania inahitaji kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
"Kuwepo kwa Vyama vingi hakumaanishi kuwepo kwa demokrasia. Msingi wa demokrasia ni watu na haki zao. Mfumo wa demokrasia unategemea mila na desturi za nchi" Alibainisha profesa Lipumba na kuongeza kuwa
Mkutano huo pia ulibainisha kwa Wadau wa demokrasia wanao wajibu wa kujenga mfumo wa demokrasia wa kushindana kwa hoja ambao hautaathiri amani na umoja wa kitaifa sambamba na kutolewa kwa Elimu bora ya uraia katika ngazi zote ni muhimu katika kuimarisha umoja wa kitaifa na kujenga demokrasia endelevu kutokanaa na kuwepo na Maadili uporomokaji wa maadili na kukithili kwa vitendo vya Rushwa na ufisadi.
Mkutano huo uliagiza kuangaliwa upya kwa Sheria ya Vyama vya Siasa ya 2019 na Sheria ya Polisi ipitiwe upya ipitiwe kwa lengo la kuimarisha demokrasia ili Jeshi la Polisi liheshimu haki za raia na liendeshwe kwa weledi na uwajibikaji kwa kutambua Haki za Vyama vya Siasa kufanya mikutano ya hadhara yenye amani na utulivu iheshimiwe ili vyama vipate fursa ya kunadi sera zao na kushawishi wanachama wapya wajiunge na vyama vyao
Kwa upande wa JITIHADA ZA KUFUFUA UCHUMI NA KUKAMILISHA MIRADI YA MAENDELEO Profesa lipumba alisema mwaka 2021 tulirejea Ushauri wetu kwa Rais Samia tuliompa mara tu baada ya kuapishwa kwake kufatia kuweka bayana msimamo wetu kama Chama kwamba kwa kuzingatia Bajeti ya nchi yetu na vyanzo vyetu vya mapato, ni kujidanganya kudai kwamba tunaweza kufanikisha Ujenzi wa Miradi mikubwa ya Maendeleo kwa kutumia mapato yetu ya ndani, bila kutegemea misaada na mikopo yenye masharti nafuu.
"Tulimshauri Rais Samia aifungue nchi Kimataifa ili kutafuta nguvu ya kifedha kwa ajili ya kufanikisha miradi hii na pia kuitangaza nchi yetu Kiutalii ambapo Rais amefanya ziara nyingi za kuitangaza nchi na kuvutia wawekezaji"
Amesema Hatimaye jitihada hizo zimezaa matunda ambapo wote mashahidi kwani tayali uamuzi wa mwisho wa uwekezaji wa Uchimbaji wa gesi ya baharini kusini ya Tanzania unatarajiwa kukamililika hivi karibuni hii ni Kufuatia jitihada hizi za kuifungua nchi Kimataifa Tanzania imeweza kupata faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata mikopo ya masharti nafuu. Mikopo hii ikitumika kwa Uadilifu na kwa kuzingatia malengo, nchi yetu itapiga hatua kubwa Kimaendeleo.
Kuhusu USTAWI WA WANANCHI NA HALI YA FURAHA KWA MWAKA 2022: Alisema jitihada za rais Samia za kuifungua nchi Kimataifa na kufanikiwa kupata fursa ya mikopo yenye masharti nafuu, wananchi wamekosa furaha na ustawi kwa sehemu kubwa ya mwaka 2022.
Ametaja sababu za kukosa furaha kwa wananchi ni kufatia Kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu ikiwemo vyakula, kukosekana kwa maji na umeme wa uhakika pamoja na mfululizo wa tozo mbalimbali ni miongoni mwa adha zinazowanyima furaha watanzania walio wengi.
Pamoja na taarifa za Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) kuonesha kuwa wastani wa mfumko wa bei ni asilimia 4.9 ambao ni chini ya nusu ya mfumko wa bei wa Kenya (9.5%) na Uganda (10.6%), gharama za maisha na hususan bei ya chakula inapanda kwa kasi ya juu wakati wananchi wengi hawana ajira na kipato cha kujikimu.
Takwimu hizo licha ya kuonyesha kuwa mfumko wa bei wa chakula ni asilimia 9.5 Kuna haja ya kufanya utafiti wa kina wa namna Shirika la Takwimu linavyokadiria mfumko wa bei na kufanya marekebisho ili pawe na uhalisia wa makadirio ya mfumko wa bei. Kasi ya ongezeko la idadi ya watu ni asilimia 3.2. Pato la taifa linakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.9. Ongezeko la kipato cha wastani wa kila Mtanzania ni asilimia 1.7.
Alisema Ili kupunguza umaskini na kuongeza ajira Tanzania inapaswa kukuza Pato la Taifa kwa alau asilimia 8 kila mwaka. Kama taifa tunahitaji Mkakati wa kukuza uchumi shirikishi unao ongeza ajira na vipato vya wananchi wa kawaida na kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.
Prof lipumba alishauri Mkakati huo ujikite katika kukuza tija ya wakulima wadogo waingie katika kilimo cha kibiashara, kuvutia uwekezaji viwandani unaoajiri vijana wengi na kutumia malighafi ya ndani. Kuongeza thamani ya madini yanayopatikana nchini.
Ametaja nyingine kuwa ni Kuvilinda na kuvitumia vivutio vya utalii kuongeza ajira ya vijana. Kuwekeza kwenye nguvu kazi kwa kuboresha elimu ya sayansi na ufundi na huduma za afya ni muhimu katika kukuza uchumi shirikishi.
No comments