Breaking News

UDSM: Yaipongeza Serikali Kwa Namna Inavyokabiliana Na Janga La UVIKO-19

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mahafali ya 51 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Jaji mstaafu Damian Lubuva akizungumza katika mahafali ya 51 ya wahitimu wa Digrii za awali, Stashahada na Astashahada  uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 

Dar es salaam:
Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeipongeza Serikali kwa hatua ilizochukua na inazoendelea kuchukua katika kukabiliana na ugonjwa wa corona unaotishia maisha ya watu na uchumi wa nchi.

Akizungumza katika Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeonesha juhudi za kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo mbalimbali kwa watanzania juu ya namna ya kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19.

Amesema wahitimu wanawajibu wa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19 ili kusiweze kupotea kwa nguvu kazi ya taifa
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa William Anangisye amesema changamoto ya UVIKO 19 imeendelea kuathiri shughuli za chuo kama vile makongamano, utafiti na pia idadi kubwa ya wanafunzi wa kigeni hawajaweza kurudi chuoni kuendelea na masomo kutokana na athari za ugonjwa huo.

Aidha ameishukuru serikali kwa kuendelea kukiwezesha Chuo ikiwemo kukipatia fedha za kuendesha shughuli mbalimbali huku akimuhakikishia Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba fedha zote chuo inazopewa na serikali zitatumika kwa matumizi ya chuo na endapo itadhihirika fedha hizo kutumika kinyume na matarajio, baraza la chuo halitosita kuwachukulia hatua kali wahusika kwani ni kinyume na sheria.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Prof. Aldin Mutembei akizungumza katika mahafali ya 51 ya wahitimu wa Digrii za awali, Stashahada na Astashahada  uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku Digrii za awali, stashahada na astashahada wahitimu katika mahafali ya 51 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

No comments