Dkt. Mpango Mgeni Rasmi Mazingira Marathon
Makamu wa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mbio za kuamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira. (Mazingira Marathon) zikazofanyika November 14 katika viwanja vya Green ground (Viwanja vya farasi) Jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini Dar es salaam juu ya maandalizi ya mbio hizo mratibu wa mbio hizo, Chief Promotions Dkt. Amon Mkonga amesema Dhumuni la mbio hizi ni kumuunga mkono Mhe Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira na Uzazi salama.
"Maandalizi yote wamekamilika hivyo kuwataka wananchi kujiandikisha kushiriki mbio hizo kwani mapato yatakayo patikana yaenda kusaidia kuboresha huduma za uzazi salama kwa lengo la kusaidia jitihada za serikali kupunguza vifo vinavyo tokana na uzazi nchini" alisema Mkonga.
Bw. Mkonga alibainisha kuwa vifaa vya kusaidia wakati wa kujifungua kwa kina mama vitasambazwa katika vituo vya afya Unguja Kusini, Tanga, Tabora na Dar es Salaam kuhakikisha anaunga mkono serikali kuhakikisha kuna kuwa na mazingira salama wakati wa kujifungua.
Chief Promotions kwa kutambua jitihada ya serikali katika kuboresha mazingira pamoja na kutambua uwepo janga la Uvico-19 pamoja na kusaidia kuboresha huduma za afya pia yatasaidia kuhamasisha kufanya mazoezi kuimarisha kinga za miili yao.
"Kukosekana huduma za msingi za afya ya uzazi kunaweza kukasababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo vya kina mama na Watoto wakati wa kujifungua hivyo hatua hii ni ya kuokoa maisha"
Gharama za kujisajili ni, 21 KM Tsh 30,000, 10Km na 5Km ni Tsh 25,000, aidha pia kwa watakao kuwa na vikundi vya Jogging Tsh 20,000, ambapo washiriki wote watapata T,shirts,Medali na Bibs namba za kukimbilia.
Mazingira Marathon imebeba Kauli Mbiu isemayo Mazingira salama ya uzazi kwa Mama, zimedhaminiwa na Kinglion na Serengeti Breweries, METL, kupitia MO Extra, Afya water, Securities Printers, TBL, Grano Coffee,Turkish restaurant, Golden Tulip Hotel.
Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii: tembelea Tovuti yetu: www.chiefpromotions.or.tz au www.mazingiramarathon.or.tztz
No comments