Breaking News

Tanzania Muslim Professional Association Wafanya Mkutano Mkuu Jijini Dar

Taasisi ya Tanzania Muslim Professional Association (TAMRO) Wamefanya mkutano mkuu wa mwaka sambamba na kufanya uchaguzi wa vingozi wake kwa mujibu wa sheria. 

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar es salaam mwenyekiti mstaafu na Katibu wa Tume ya Uchaguzi wa chama hicho Bw. Pazi Mwinyimvua Amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo pia utapiga kura kupata viongozi wapya ngazi ya mbalimbali kama inayoelekeza katiba yao.

"Chama chetu ni chama cha wanataaluma leo tumekutana kujadiliana na kubadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali yanayohusu chama pamoja na kuchagua viongozi wapya mara baada ya viongozi waliokuwepo kumaliza mda wao kikatiba" Alisema bw. Mwinyimvua

Alisema katika mkutano huo pia kila mjumbe atapata nafasi ya kushiriki uchaguzi ambao utawapata viongozi watakao ongoza kwa kipindi kingine baada ya waliokuwepo kumaliza mda wao kisheria.

Mkutano huo umefanyika katika hotel ya Golden Tulip City Central jijini Dar es salaam

No comments