Breaking News

TBS Yatoa Ufafanuzi Juu Ya Juice Ceres Yenye Sumu Kuvu

Shirika la Viwango TBS limewatoa limetoa ufafanuzi na kuwatoa hofu wananchi kufatia sintofahamu kufatia juice ya Ceres ya inayotokana na tunda la apple kutoka Afrika Kusini kuripotiwa kuwa na sumu Kuvu imesema kuwa juice hizo hazijaingia Tanzania.

Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Dar e s salaam Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga Amesema kuwa kimsingi taarifa inayosambaa mtandaoni ni taarifa ya awali ya mzalishaji ambayo uitoa endapo bidhaa aliyoisambaza kwa wateja wake ina hitilafu yoyote, na taarifa hiyo hutolewa kupitia mtandao wa kimataifa wa mamlaka ya uthibiti usalama wa chakula ambao nchi 196 ni wananchama.

"Taarifa ambayo inasambaa mtandaoni ni taarifa ya awali ya mzalishaji ambayo uitoa endapo bidhaa aliyoisambaza kwa wateja wake ina hitilafu yoyote, na taarifa hiyo utolewa kupitia mtandao wa kimataifa wa mamlaka ya uthibiti usalama wa chakula" Alisema Bw. Msasalaga

Alisema Tanzania ni Moja ya nchi wanachama hivyo mzigo ulionekana kuwa na sumu Kuvu bado haujaingia nchini, kwa kulihakikisha hilo TBS ilimtembelea Wakala wa uagizaji wa juice hiyo nchini na kukagua mzigo na kukuta mzigo wenye hitilafu za kiusalama wa kuanzia Toleo la Juni 14 - 30, 2021 haujaingia nchini Bali ni nchi za Kenya, Jamhuri ya Congo, Zimbabwe na nyinginezo.

Aidha Bw. Msasalaga aliongeza kuwa mzigo ambao unatarajiwa kuingia nchi wa Toleo hilo utateketezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za mamlaka hiyo

No comments