KiKWETE Aupongeza Uongozi wa Chuo Cha UDSM Kwa Kupiga Hatua Katika Usawa wa Jinsia Kwa Wahitimu
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Rais Mstaafu mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kupiga hatua katika usawa wa jinsia kwa wahitimu wa shahada za waliohitimu chuoni hapo mwaka huu wa masomo 2021.
Pongezi hizo amezitoa wakati akiwatunuku vyeti wahitimu wapatao 4121 wa awamu ya pili katika ngazi ya digrii akisema kuwa amefurahishwa na idadi ya wanafunzi wa kike kuongezeka mwaka hadi mwaka na kuutaka uongozi wa UDSM kuhakikisha usawa wa kijinsia kwa wahitimu unafikia asilimia 50 kwa 50.
"Nimesikiliza hotuba yako Makamu mkuu wa chuo nimefurahishwa na takwimu kwamba wahitimu wote wapo 4121 lakini kati ya wanaume ni 2101 na wanawake i 1920, hatua hii ni nzuri sana, usawa wa kijinsia kwa wahitimu wa shahada za awali unaonekana kupanda hivyo nawapongeza sana kwa hatua hiyo," alisema Dkt. Kikwete.
Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dr. William Anangisye amesema kwamba chuo hicho kimepata mafanikio makumbwa ikiwemo kupata kiasi cha Billioni 3 kwa ajili ya kufanya utafiti na ubunifu,pamoja nakuanza kudahili wanafunzi kutoka mataifa yakigeni kwa ajili yakujifunza lugha ya kiswahili.
Hata hivyo Profesa Anangisye amewaasa wahitimu hao Kuwajibika kwa kutumia elimu zao kuwa na ushawishi wa kuleta chachu ya maendeleo katika Taifa na Dunia kwa ujumla, kufanya kazi kwa bidii, pamoja na kuendelea kujifunza mambo mapya na sio kubaki nyuma.
"Tuna wapongeza sana mnaohitimu leo, lakini napenda niwakumbushe msiende kutegemea kuajiriwa serikalini,bali mkawe chachu yakutengeneza ajira, mfanye kazi kwa bidii, muwe na nidhamu kazini, mjiendeleze kimaarifa lakini pia mkipata nafasi za kazi za kujitolea mfanye ili mjijengee uzoefu nankujiami, kwahiyo msikate tamaa mnapokumbana na changamoto mbalimbali za kazi" amewaasa Profes huyo.
Nae Mwayekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM) Jaji Mstaafu Damian Lubuva ameshukuru hatua zinazo chukuliwa na Rais Samia kujikinga na uginjwa wa Uviko 19, nakutumia fursa hiyo kusema kuwa chuo kinaendelea kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.
"Nyinyi wahitimu na wale mnaobakia nawaomba muendelee kuchukua tahadhali kama tunavyoelekezwa na wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa wa uviko 19, rais amekuwa mstari wa mbele kutukumbusha haya na sisi tuendelee kumuunga mkono" amesema Jaji Mstaafu Lubuva.
Jumla ya wahitimu 4121 wanahitimu katika ngazi ya cheti Shahada na Astashahada katika mahafali ya 51 ya Chuo kikuu cha Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jiijini Dar es salaam.
No comments