Breaking News

TASAF Yatoa Mchanganuo Namna Bil 5.5 za Utekelezaji wa Mpango Wa Maendeleo Kwa Ustawi Zitakavyotumika

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeeleza namna ambavyo kiasi cha Bilioni 5.5 zitavyo elekezwa katika utoaji wa Ruzuku na utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa kaya za walengwa ili kupata kipato kitakacho ziwezesha kaya Hizo kujikwamua kiuchumi na kupunguza athari za UVIKO 19.

Ufafanuzi huo umetolewa Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw Ladislaus Mwamanga wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa mpango wa kunusuru Kaya za walengwa wa TASAF.

Bw. Mwamanga alisema kupitia fedha hizo kaya za walengwa 40,740 wenye uwezo wa kufanya kazi ambao wanaishi katika maeneo ya Mijini, watafanya kazi katika miradi ya Jamii na Kulipwa ujira wa wastani wa Tsh 135,000 kwa kila kaya ili kufufua na kuimarisha shughuli zao kukuza uchumi wa kaya zao.

“TASAF itazitumia fedha Hizo kuondoa athari za kiuchumi zilizochochewa na mlipuko wa UVIKO -19 kwa kaya za walengwa wa TASAF ambao serikali imedhamiria kuwaondoa katika umaskini wa kipato kwa kuwapatia Ruzuku za kujikimu, Ajira za muda, kuwaongezea ujuzi, maarifa na elimu ya ujasiriamali" Alisema Bw. Mwamanga.

Alisema serikali ya wamu ha sita Inayoongozwa na mhe. Mama Samia Suluhu Hassani itaendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali katika kupunguza umaskini wa watanzania wanaoishi kwenye mazingira duni na inafanya jitihada kubwa kupata fedha kutoka vyanzo vya ndani.

“Utoaji wa sehemu ya Mkopo huu nafuu kwa ajili ya mpango wa TASAF ni kielelezo tosha kwamba serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi wake hasa wale wanaoishi katika mazingira duni”amesema Mwamange

Aidha Bw. Mwamange aliongeza kuwa Menejimenti ya TASAF kwa mwongozo wa Kamati ya Uongozi ya Taifa itahakikisha inasimamia maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa walengwa katika maeneo yatakayo ainishwa unaanza mara tu baada ya fedha Hizo kupokelewa.

"Katika kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kama ilivyo kusudiwa kutakuwa na usimamizi makini kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango kulingana na thamani ya fedha".

 

No comments