Breaking News

DC LUDIGIJA: Wazazi na Walezi Wenye Watoto Wenye Vichwa Vikubwa na Mdomo wazi Kufika Viwanja Vya Mnazi Mmoja Oct 22

Mkuu wa wilaya ya mhe. Ngw'irabuzu Ludigija amewataka wazazi na walezi wenye watoto walio na vichwa vikubwa  na mdomo wazi kufika katika viwanja mnazi mmoja siku ya tarehe 22 octoba kuweza kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu.

Kizungumza jijini Dar es salaam kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Watoto Wenye Vichwa vikubwa na Mdomo Wazi alisema katika siku hiyo huduma za vipimo na matibabu kwa watoto wenye tatizo hilo zitaolewa bure.

"Naomba nitoe wito kwa wazazi na walezi ambao wanaishi na watoto wenye vichwa vikubwa na mdomo wazi hususani wanaishi mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi terehe 22 mwezi huu katika viwanja vya mnazi mmoja " 

Alisema katika kuadhimisha siku hiyo mwaka huu watoto wenye vichwa vikubwa na mdomo wazi watapatiwa huduma ikiwemo vipimo pamoja na ushauri.
 

No comments