Breaking News

Ni Mbavu Misuli hekaheka Kama zote !! Mshindi Mr Tanzania 2021 Kupatikana Alhamisi hii

Niwale jamaa wenyembavu za misuli  wiki Alhamisi Kamati ya mashindano ya MR Tanzania imesema siku hiyo ya October 22 mwaka  huu, washiriki wote wa Mr . Tanzania watatakiwa kuripoti katika ukumbi wa Kilimanjaro, Ubungo Plaza Dar es Salaam siku hiyo kuanzia saa 7:00 asubuhi.

Akizungumza kuhusiana na shindano hilo Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo huo toka    (TBBF ) Francis Mapugilo amesema  wanatarajia Shindano litakuwa Katika hekaheka tofauti Kwa kuwa washindi watakaoibuka siku hiyo dhamani yao mbali na kupata zawadi yapo malengo mengi yenye fursa katika sanaa hiyo .

Wameamua kufanya shindano hilo pekee tuu kwa mwaka huu kutokana na mdhamini kushindwa kumudu gharama za Mr Tanzania, Mr Physique .

Amesema kamati imeomba radhi sana washiriki ambao vipengele vyao hivyo vitakosekana kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wa kamati.

"Kwa watu waliotayari kugombea watalipa Tsh 100,000 (Shilingi Laki Moja tu) na Mpesa Kwa  0753559833 (Chandrakanta Asawla) na mara tu malipo yatakapo kamilika ,utapokea ujumbe wa malipo nyenye kupokelewa ndani ya masaa 24,"amesema Mapugilo.
Amesema kwa waliona Tigo wanaweza kutuma Kwa 0653 215757 kwa Rishabh Patel ambapo fomu zinapatikana kwenye wavuti yao www.tzbbf.org katika safu ya usajili pia unaweza kuipakua Kwa bure.

Katibu huyo amesema kuwa fomu pia zinapatikana katika kumbi za michezo mbali mbali Jijini Dar es Salaam maenei ya Gym Bodyline Mikocheni, Gym Home Mwenge, Body Fuel Masaki  pamoja na Gym zingine.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Pilipili Intertainment Millesh Batt, ambao ndio waandaji washindano hilo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo huku kwa wale ambao hawatobahatika kufika ukumbini.

"Uhakika ni hivi bodybuilding safari hii itakuwa ni (Free Class) kwa maana hakutakuwa na groups kutokana na uzito wao ."amesema Mapugilo

Amesema wamefanya hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti ya mashindano , na kutakuwa na kipengele cha best Poser ilikuleta ladha kwenye shindano .

Zawadi kwa washindi zimetajwa kuwa ni kemkem ilikuchochea amasa katika shindano hilo.

Na  Timothy Marko

No comments