Breaking News

UDSM Yaadhimisha Miaka 60 Kwa Kutoa Msaada Katika Sekta ya Afya

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Bearice Dominic akipokea mashuka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye katika Kituo cha Afya cha Kimara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic akifafanua jambo katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya Hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara Jijini Dar ees Salaam.

Dar es salaam:
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo octoba 25 kimetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1961 miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika kituo cha afya Kimara.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kisaada hiyo Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa William Anangisye amesema taasisi hiyo kama sehemu ya jamii imeamua kuadhimisha siku hiyo kwa kuikumbuka jamii.

Profesa Anangisye amesema chuo kimetoa msaada huo kama alama ya UDSM katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho kikongwe na maadhimisho hayo yatafanyika ndani ya mwaka mmoja kuanzia leo

Amesema wakati chuo hicho kinaanzishwa kulikuwa na kitivo cha sheria pekee ambacho kilikuwa na wahadhiri sita akiwemo mwafrika mmoja, wanafunzi 14 akiwemo mwanamke mmoja.

"Wakati chuo kinaanzishwa kilikuwa na kitivo cha sheria tu ambacho kilikuwa  na wanafunzi 14 wakiwepo mmoja wa kike ila kwa sasa kina wanafunzi 43307,Kati ya hao wanafunzi wa kike ni 19784 sawa na asilimia 45.7 katika mwaka wa masomo 2021"

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amesema msaada huo una tija kubwa kwenye kituo hicho.

“Mlichofanya leo kwetu ni kikubwa sana kama mnavyoona hali ya kituo hiki, mahitaji ni makubwa ukilinganisha na uwezo tulionao.

Alisema kipekee tunashukuru UDSM kwa kuendelea kuibeba manispaa ya Ubungo nawahakikishia vifaa hivi ambavyo vimekabidhiwa leo tutavitunza kuhakikisha vinabaki kwenye ubora wake

Aidha Mkurugenzi huyo  aliomba msaada wa  chuo hicho kuhusu suala la kuwapanga wamachinga na kuomba  chuo kutekeleza mpango huo.

“Nilikuwa najiuliza hivi kwanini nahangaika na wamachinga wakati kuna wasomi ambao wanaweza kututengenezea au kushauri muundo wa kitaalam wa namna ya kufanya biashara".

Halmashauri ina kazi kubwa ya kupanga wamachinga, tunaomba msaada tutumie watalaam wa UDSM kuangalia namna bora ya kuwapanga hawa machinga,” alisema Beatrice.
Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Bearice Dominic akipokea kiti cha mgonjwa kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye kwa ajili ya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kimara Jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam utafiti, Prof. Benadeta Killian akitoa historia ya chuo katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara Jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt.Peter Nsanya akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya katika Kituo cha Afya cha Kimara Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic (katikati) akiwa pamoja na  baadhi ya Viongozi wakipata picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walioweza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.

No comments