Breaking News

RC MAKALLA: Tunapo Ombea Amani Tanzania.. Tumwombee na Mama SAMIA Agombee 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Viongozi wa Dini wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi mikutano Sita ya injili  katika wilaya 5 za mkoa wa Dar es salaam  mikutano itakayo ongozwa na  Muhubiri wa kimataifa mwinjilisti Daniel kolenda.

RC Makalla ametoa wito wakati wa Mkutano na Viongozi wa Dini akimuwakilisha Rais Samia kuelekea Mikutano mikubwa ya Imani, Upendo na Miujiza itakayofanyika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es salaam ambapo alisema kuwa Taifa limepata kiongozi imara alieonyesha dira nzuri ya kuifikisha Tanzania Kwenye Hali nzuri kisiasa, kiuchumi na kijamii.

"Naomba ntoe rai kwa wachungaji wanaoofanya  Maombi ya kuliombea Taifa Amani, Upendo na Mshikamano pia wamuombee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  awe Na afya njema Na agombee  uraisi ifikapo mwaka 2025."

Alisema Miongoni mwa sababu zinazofanya Rais Samia astahili kugombea Uraisi 2025 Ni pamoja na Mwendelezo wa Elimu Bure, Ongezeko la Mapato, Utekelezaji wa Miradi Mikubwa ya maendeleo ikiwemo Barabara, Bandari, Shule, Hospital, Maji na mingineyo.

Aidha aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwaheshimu na kuwajali Viongozi wa Dini kwakuwa wamekuwa chachu ya kuhubiri Amani, Upendo na Mshikamano miongoni mwa Wananchi jambo linalopelekea Tanzania kuendelea kuwa kisiwa Cha Amani.

Nao Viongozi wa Dini akiwemo Mwangalizi Mkuu wa Wapo Mission international Askofu Sylvester Gamanywa amemtia moyo Rais Samia Suluhu Hassan na kueleza kuwa Viongozi wa Dini Wana Imani kubwa na yeye pamoja na Serikali anayoiongoza.

"Mikutano ya injili ya Imani, Upendo na Miujiza inafanyika Katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Kawe, Kimara, Gongolamboto, Mbagala, Jangwani na Kigamboni kuanzia October 06 saa 9 Mchana Hadi saa 12 jioni" Alisema Askofu Gamanywa
 

No comments