Breaking News

Serikali Yaandaa Mfumo Wa Kidijitali Kwa Ajili Ya Uchambuzi Wa Hali Ya Hewa

Katibu Mkuu, Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana Na Wenye Ulemavu), Mhe. Tixon Nzunda akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Oktoba 13, 2021.

Na Emmanuel Mbatilo, Dar Es Salaam
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeanda  jukwaa la mfumo wa kidigitaji kwa ajili ya uchambuzi wa hali hewa ili kubaini madhara ya mafuriko na ukame kwa wakati.

Katibu Mkuu, Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana Na Wenye Ulemavu), Mhe. Tixon Nzunda akitoa taarifa Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Oktoba 13, 2021.

Mhe. Nzunda alisema Serikali imeandaa mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa katika halmashauri 20 zilizoonekana kuwa katika hatari kubwa ya kuathirika na maafa.

"Halmashauri zilizoandaliwa mipango ya dharura ni Chamwino, Kondoa na Mpwapwa katika Mkoa wa Dodoma; Shinyanga Vijijini na Kishapu katika Mkoa wa Shinyanga; Bariadi, Maswa na Meatu katika Mkoa wa Simiyu); Mwanga na Same katika Mkoa wa Kilimanjaro; Kilosa, Mvomero na Kilombero katika Mkoa wa Morogoro; Mtwara Manispaa, Halmashauri ya Mtwara na Masasi katika Mkoa wa Mtwara; Bukoba Manispaa, Bukoba halmashauri katika mkoa wa Kagera; Meru katika Mkoa wa Arusha; na Liwale katika Mkoa wa Lindi".  Alisema Mhe. Nzunda.

Mhe. Nzunda alisema Menejimenti ya maafa nchini inazingatia utaratibu wa uhusiano wa kisekta unaotoa ushiriki thabiti na utangamano na wadau wote. Majukumu ya utendaji yanazingatia taasisi yenye wajibu wa kisheria, ujuzi pamoja rasilimali zinazohitajika.

"Kila sekta inawajibika kutambua hatari za maafa katika eneo lake, kutenga rasilimali kabla ya tukio na kujenga uwezo wa kukabili kuanzia ngazi ya taifa, mikoa, wilaya, kata, kijiji na jamii. Majukumu ya jumla kwa makundi mbalimbali". Alisema Mhe.Nzunda.

Alisema Wizara, idara na taasisi zinapaswa kuongoza juhudi za kupunguza madhara ya maafa pamoja na kusimamia hatua za kukabiliana na dharura kwa kutumia rasilimali zake. Sekta zinapaswa kuchukua hatua za kuainisha majanga, kutathmini hatari, kufuatilia na kuchukua hatua kupitia mipango na bajeti zake.

Aidha Mhe. Nzunda aliongeza kuwa Sekretarieti za Mikoa zina jukumu la kuainisha vipaumbele vya kupunguza madhara ya maafa, kuandaa mikakati, kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa masuala ya maafa katika ngazi za halmashauri. Sekretarieti za Mikoa zinapaswa kushirikisha Kamati za za Usimamizi wa Maafa ili kuimarisha uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau.

No comments