Breaking News

RC MAKALLA Awaeleza Makamanda wa Chuo Cha Kijeshi Kuwa DSM Ina Viwanda Vingi Na Shughuli za Kiuchumi.

- Ampongeza Rais Samia Suluhu Hasan kwa hatua alizochukua katika kipindi Cha miezi 6 kukuza uchumi, kuvutia watalii Na Wawekezaji na utalekelezaji wa Miradi mingi ya maendeleo.

- Makamanda waridhishwa na hatua za Serikali kuvutia wawekezaji kwa kupunguza tozo, Mamlaka za udhibiti kuwa sehemu moja na utekelezaji wa Blue Print.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelewa na ugeni wa makamanda wa Kijeshi kutoka Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu CSC Duluti Cha Mkoani Arusha waliokuja Dar es salaam kwa ziara ya kujifunza Masuala ya uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo endelevu.

Ugeni huo unajumuisha makamanda wa Vyeo vya juu vya  Kijeshi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Misri, Burundi, Malawi, Zimbabwe, Kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania

Akizungumza na Makamanda hao, RC Makalla ametumia nafasi hiyo kueleza jitiada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita Katika kuboresha na kuweka mazingira Bora ya Uwekezaji na biashara ikiwemo uanzishwaji wa one stop Center ya Biashara ya Mkoa huo ambayo inakwenda kupunguza Urasimu.

Aidha RC Makalla amewapongeza Makamanda hao kwa uamuzi sahihi wa kuchagua Mkoa wa Dar es salaam Kama sehemu ya mafunzo na amewahakikishia usalama na ushirikiano kwa muda wote watakaokuwepo Dar es salaam.

Ugeni wa makamanda hao unaongozwa na Brigedia Jenerali Sylvester Damian Ghuliku ambae ni Mkuu wa chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Duluti Cha Mkoani Arusha na watatembelea maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

No comments