TBS Yawataka Wazalishaji wa Matofali Kuzingatia Viwango
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wazalishaji na watengenezaji wa matofali ya saruji na mchanga kuhakikisha wanakutengeneza bidhaa hizo kwa viwango vilivyowekwa ili kumlinda mtumiaji aseweze kupata madhara
Akizungumza leo Oktoba 8, 2021 na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika hilo, Bwana Aziz Msemo amesema kuwa katika mchakato wa uandaaji wa viwango kuna kuwa na mpango wa taifa wa wauandaaji wa viwango ambao unahainisha bidhaa ambazo zikitumiwa na Watanzania zinaweza kuleta athari kiafya, uchumi au Usalama wa Nchi, hivyo kuwepo viwango katika Matofali itasaidia sio tu kwa watumiaji hata kwa watengenezaji ambapo itafungua fursa za kibiashara nje ya Mipaka ya Nchi.
Akieleza kuhusiana na dhumuni la TBS kuandaa viwango vya matofali amesema kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kulinda usalama wa Watu tofauti na jengo endapo litajengwa na matofali yenye viwango duni majanga yakitokea kama vile ya tetemeko na mtikisiko inaweza kuelekea madhara na hasara ya kiuchumi kwa wananchi.
“Bidhaa ambayo haina ubora ukiitumia leo na kuharibika utahitaji kununua nyingine kwahiyo utakuwa haujazingatia suala lla uchumi hivyo kwa upande wa matofali pale unapojenga jengo ambalo matofali yake hayana ubora unaotakiwa basi utahitajika kufanya matengenezo mara kwa mara kwenye hilo jengo,” Amesema Bwana Msemo.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wana kiwango no. TZS 283 ambacho kinaianisha matakwa ya matofali ambayo yanatengenezwa kwa simenti na mchanga ili kuweza kuhakikisha mtumiaji asiweze kupata madhara.
Aidha Bwana Aziz Msemo amesema Shirika la Viwango (TBS) linawataka wazalishaji wa bidhaa za matofali wote kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kwani kwa kufanya hivyo itawawezesha kuaminika na kupata masoko mapya ndani na nje ya mipaka ya Nchi.
No comments