Rc Makala Aongeza Mda Wa Machinga Kuondoka Hadi Octoba 30
Na Timothy Marko, Dar es salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makala amewataka watendaji wa wilaya katika mkoa huo Kuhakikisha vibanda vya wamachinga vinaondolewa Hadi kufikia October 30 Mwaka huu.
Akizungumza katika kikao cha watendaji wa jiji Hilo mkuu wa Mkoa Amos Makala alisema ni lazima watendaji Kuhakikisha hifadhi ya Barabara inakuwa Safi.
"Ninatarajia mpaka kufikia tarehe 30 mwezi huu sitaona kibanda chochote kwenye hifadhi ya Barabara".Alisema Makala.
Mhe. Makala katika hatua nyingine amewataka watendaji kuhakikisha wanayafanyia usafi maeneo ambayo tayali wamachinga wameondoka pamoja na kuweka ulinzi hususani nyakati za usiku.
Aidha Rc Makala amesisitiza kuwa Wafanyabiashara hao kuondoa vibanda hivyo wenyewe katika maeneo ya hifadhi ya barabara na juu ya mitaro ya maji taka.
Ametangaza ma DC, wakurugenzi watendaji wa mitaa na kata kusafisha jiji katika maeneo waliyohama wamachinga. Hataki kuona kibanda wala biashara katika maeneo ya watembea kwa miguu, hifadhi ya Barabara, Shule, Vyuo, na maeneo muhimu
"Nitaka ifikapo octoba 30 mitaro yote kwenye Barabara inakuwa wazi sambamba na Maeneo yote ya watembea Kwa miguu ". Aliongeza Makala
No comments