Breaking News

Mawakala Wa Forodha Waiomba Serikali Kufanyia Kuzipitia Baadhi za Sheria za Sekta Hiyo

Timothy Marko
Mawakala wa Forodha nchini wameiomba Serikali kupitia taasisi inayoshugulika na udhibiti  Masuala ya Forodha (TASAC) kuendelea na majukumu yake na kutoendelea na uwakala wa sekta hiyo.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Sprint Cargo limited inayo jishughulisha na masula ya Forodha, Bw. Robert Mushi ameiomba Serikali kufanyia Marekebisho ya sheria ya sekta hiyo ili kuleta ufanisi katika Uchumi kupitia sekta hiyo.

"TASAC anapokuwa mdhibiti wa taarifa za kiforodha halafu hapo hapo anakuwa wakala hii  haiposawa". Alisema Mkurugenzi Rorbet Mushi.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya Ikumo clearing forward inayo jishughulisha na masula ya Forodha, Bw. Ikupa  Njela amesema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto ikiwemo ushindani na upatikanaji wa kazi zinazo husiana na sekta hiyo
Alisema TASAC ambayo ni mdhibiti wa Masuala ya Forodha imechukua kazi nyingi za Forodha.

"Hali hii inafanya Biashara kuwa ngumu, hata ulaya kutokana na janga Uviko Hali ya Kufanya kazi imekuwa hafifu". Alisema  Njela .

No comments