Breaking News

Washiriki Taji La Miss Kanda Ya Mashariki Watoa Msaada Hospitali Ya Tumbi Pwani

Mwandaaji wa shindano la kumsaka miss kanda ya mashariki Injinia Nancy Matta akikabidhi msaada walipofanya ziara na walimbwende katika hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ikiwa ni katika kuelekea katika shindano hilo litakalofanyika septemba 24 mwaka huu mjini morogoro
Mwonekano wa baadhi wa warembo ambao wanatarajia kupanda jukwaani mjini morogoro septemba 24 mwaka huu wakiwa nje ya hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi walipo kwenda kutoa msaada  katika wodi ya wakinamama.(PICHA Na VICTOR MASANGU

PWANI
WALIMBWENDE wanaotarajia kushiriki katika kuwania taji la shindano la miss kanda la mashariki kwa mwaka huu wa 2021 wamefanya ziara maalumu kwa ajili ya kutembelea katika Hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi kwa lengo la kuwafariji wagonjwa  mbali mbali  katika wodi ya wakinamama na kuwapatia  msaada wa sabuni.

Akizungumza na waandishi wa habari Hospitalini hapo mara baada ya kutoa msaada wa sabuni mratibu wa shindano hilo Injinia Nancy  Matta alisema kwamba  katika kuelekea kinyng’anyiro hicho warembo hao wameamua kwenda kutoa msaada katika wodi ya wakinamama kutokana kuwepo kwa mahitaji mbali mbali hasa wakati wa kujifungua.

Injinia Nancy aliongeza kuwa anatambua chanagmoto mbali mbali ambazo zinawakabili waakinamama hasa katika kipindi cha kujifungua hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa ya kwenda kuwatembelea wagonjwa hao katika hospitali  hiyo  ya  tumbi pamoja na kuwafariji nia ikiwaa ni kutoa kile kidogo walichonacho.

Katika hatua  nyingine  Nancy  aliongeza kuwa   shindano hilo  la miss kanda ya mashariki ambalo linatarajiwa kufanyika  septembe 24  mwaka huu  mjini  morogoro na kwamba litakuwa la aina yeke  na ushindani mkubwa kutokana na warembo wote kujiandaa vya kutosha na kuwataka wapenzi na mashabiki wa ulimbende kujitokeza kwa wingi  siku hiyo.

Naye  Mratibu wa shindano hilo Ramaddhani Mzandete alisema kwamba kwa sasa maandalizi yote kwa ajili ya shindano hilo yanakenda vizuri na kwamba warembo ambao wanashiriki katika mchuano huo wametoka kutoka mikoa mine tofauti, ikiwemo Lindi, Mtwara, Pwani pamoja na Mkoa wa Morogoro.

“Kwa sasa warembo wapo kambini na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuijandaa na shindano hilo na kitu kikubwa sisi kama viongozi pamoja na washiriki tumeweza kuja katika hospitali hii ya tumbi kwa lengo kubwa ni kuja kutoa msaada wa sabuni kwa wagonjwa hasa kwa wkinamama ambao wamejifungua,”alisema mratibu huyo.

Kwa upande wake  Enjolata Mtitu ambaye ni daktari wa wodi ya wakinamama katika hospitali ya Tumbi amesema kwamba amefarijika sana kwa ujio wa warembo hao kwenda kuwatembela na kutoa msaada wa sabuni mbali mabali katika wodi ya wakinamama na kuongeza kuwa vitaweza kuwasaidia katika mahitaji yao.

Aidha Daktari huyo alitoa pongezi zake za dhati kwa mwandaaji wa shindano hilo la miss kanda ya mashariki kwa kuweza kuona umuhimu wa kutenga muda yeye pamoja na warembo hao kwenda kuwatembelea na kuwapatua msaada huo wa sabuni na kwamba amewaomba kuendelea na moyo huo huo wa kusaidia watu wenye mahitaji mbali mbali hasa wakinamama.

No comments