Anezylitta Yaazimisha Miaka 5 Kwa Kuzindua Duka Jipya la Mapishi na Mapambo
Jamii imeombwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwasaidia katika maisha yao.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Anezylita Bi. Zena Shariff Scaba wakati wa uzinduzi wa duka lake jipya ambalo linajihusisha na masuala ya mapambo ya nyumbani pamoja na shule ya mapishi ya keki.
Kampuni hiyo ambayo ilikua inafanya mashindano ya kupika keki ambapo mwaka jana na mwaka huu hayajafanyika kutokana na ugonjwa wa korona, ambapo mashindano hayo yataanza hivi karibuni.
Bi Zena amewambia wanahabari kwamba vijana waliopo nyumbani watapata mafunzo ya mapishi na kupatiwa vyeti vya serikali ya Tanzania hivyo amewataka wachangamkie fursa hiyo.
"Tumeamua kufungua duka jingine ili vijana wajifunze mapishi lakini pia kuuza mapambo ya majumbani kwa gharama nafuu sana, wananchi wajitokeze kutumia fursa hii" amesema Bi Zena.
Aidha amesema kuwa kampuni yake imewezesha kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira.
Hata hivyo ameiomba jamii itumie vizuri mitandao ya kijamii kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kutumia kama njia ya kutangaza biasha zao.
No comments