Breaking News

WADAU WA FILAMU WATAKIWA KUWA TAYALI KUPOKEA MATOKEO YEYOTE WATAKAYOPATA KUPITIA TUZO ZA FILAMU 2021

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizaya ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Hassan Abbas tarehe 27 Septemba, 2021 alipokuwa akizungumza na Kamati ya Tuzo za Filamu 2021 (Tanzania Film Festival Awards 2021), katika kikao cha kumpitisha kuhusu muendelezo wa mchakato wa Tuzo hizo hadi sasa. 

"Washiriki wajiandae kushinda au kushindwa kwasababu kumekuwa na tabia ya kutokukubali matokeo na kusababisha walioshindwa kuwazungumzia vibaya Waandaji wa Tuzo au mashindano husika, hivyo Shirikisho la Filamu Tanzania na Vyama vyake viwaandae Wadau wetu katika kupokea matokeo" alisema Dkt. Abbas.

Akiendelea kufafanua Dkt. Abbas alieleza kuwa, Tuzo hizo ziwe na Dhana ya Utaifa, ambapo zitumike kuwa sehemu ya kutangaza Nchi na kusaidia Wadau wa Filamu kutambua masuala ya Uzalendo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo alimweleza Katibu Mkuu kuwa, lengo la kuanzisha Tuzo hizo ni kutambua mchango wa Wanatasnia ya Filamu katika utendaji wa kazi zao, pamoja na kuhamasisha utengenezaji wa Filamu bora kupitia uwekezaji unaoendelea kufanyika katika Tasnia hiyo. 

Kaulimbiu ya Tuzo hizo ni FILAMU NI BIASHARA ikiwa na lengo la kubadilisha mtazamo wa Filamu za Kitanzania kibiashara katika Masoko ya ndani na nje ya nchi. Aidha, kilele chake kinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka  2021.

No comments