Breaking News

Serikali Kuendelea Kutoa Mafunzo ya Ufundi Stadi Kwa Vijana Kukabiliana na Ukosefu wa Ajira

Na: Timothy Marko
KATIKA Kuhakikisha tatizo la ajira kwa vijana linatokomezwa, Serikali imesema itaendeleza mafunzo ya ufundi Kwa kundi Hilo illi kuweza kujiajiri na kuajirika.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Vijana kuthibitisha Rasimu ya Sera ya maendeleo ya taifa jijini Dar es Salaam Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu  bw. Julias Tweneshe alisema takwimu zinaonyesha kuwa Hali ya mahitaji ya vijana nchini imekuwa ikiongezeka siku Hadi siku ambapo  asilimia 31.5 ya watu waliopo nchini ni vijana Sawa na Asilimia 57 ya nguvu kazi ya Taifa.

"Serikali Katika Kuhakikisha kundi hili linapewa kipaumbele kuweza kuchangia Uchumi wa nchi Serikali imeunda sera vijana ya Mwaka 1996 inayo wahiza vijana kujitolea" Alisema bw Tweneshe.

Alisema katika Marekebisho ya sera hiyo  iliyofanyika 2007 sera hiyo ililenga kitenga Maeneo  Maalumu  ya kiuchumi kwa vijana.

Tweneshe aliongeza kiwa katika Kuhakikisha masuala ya vijana yanazingatiwa Serikali Imetenga Asilimia 10 kwa ajili ya mikopo kwa vijana kwa kila halmashauri ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Aliongeza kuwa katika sera Mwaka huu imelenga kutatua changamoto za kukuza ujuzi kwa ngazi kitaifa na kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa community Harb Foundation, Paul Makoe amesema rasmu ya awali ni tofauti na Mwaka huu ambayo imeongezewa vipengele vya watu wenye ulemavu na ajira zimeanza kuwainua vijana.
 

No comments