Breaking News

FCNRFG: Bado Jamii Ina Uelewa Mdogo Juu ya Utunzaji wa Mazingira

Shirika lisilo la kiserikali la mazingira (FCNRFG) lililopo kigamboni Dar es salaam limefanya tafiti na kubaini chanzo cha uharibifu wa mazingira unaofanywa katika eneo la Kibugumo unatokana ukosefu wa elimu ya mazingira.

Matokeo ya tafiti hiyo imekuja baada ya shirika hilo kufanya ziara ya kuangalia shughuli za kibinadamu za uchimbaji wa kokoto na utupaji wa takataka na kupwlwkea kuharibu mazingira ya eneo hilo.

Hayo yamebainishwa na katibu wa shirika hilo Omary Kalekela wakati walipotembelea maeneo ya Kibugumo na kubaini wakazi wengi kufanya shughuli ambazo walidai kupewa idhini na viongozi wa eneo hilo.

"Miundo mbinu ya mazingira yaliyoharibiwa na wakazi wa kibugumo yametokana na baadhi ya viongozi waliopewa dhamana na Serikali katika kuwaonfoza wananchi." alisema Kalekela

Aidha shirika hilo lilibaini chanzo kikubwa ni umasikini pamojana wananchi kukosa elimu ya mazingira hivyo kutokakana na changamoto hiyo wadau ambao ni viongozi wa maeneo ya kigamboni akiwemo mkuu wa wilaya kutupia jicho kwenye maeneo yanayoonekana kukithiri shughuli za kibinadamu.

Kalekela ameiomba Serikali ya awamu ya sita kwa kusaidiana na mashirika ya mazingira kutupia nguvu zao lwa kuielisha jamii sambamba na utoaji wa mikopo kwawakazi hao amvao malalamiko yao ni ukosefu wa kazi za kujipatia vipato.

Hata hivyo ufumbuzi wa suala hilo ni kuwawezesha wananchi katika shughuli mbalimbali zitakazo ondoa ugumu wa maisha,uwezeshwaji,shughuli halali za kujipatia vipato halali,viongozi wahusika kuwa makini na sera za mazingira na kuona umuhimu wake.


No comments