Breaking News

Rose Muhando, Martha Baraka na Martha Mwaipaja, Ndani ya Jukwaa Moja Tamasha la Kumshukuru Mungu

Maandalizi ya Tamasha la Kumshukuru Mungu ambalo limeratibiwa na Kampuni ya Msama Promotions yanaendelea vizuri huku waimbaji wa kitaifa wa nyimbo za injili wakiendelea kuthibitisha ushiriki wao.

Akitoa taarifa ya juu ya maandalizi hayo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Alex Msama alisema tamasha hilo ambalo litafanyika oktoba 31 katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Alisema Maandalizi yanaendelea vizuri na waimbaji tayari wapo kambini wanaendelea na mazoezi, kwani siku ya tamasha wataimba live kwa asilimia tofauti na ilivyo kubwa miaka ya nyuma, kufanya tamasha la mwaka huu kuwa la aina yake.

"Tunatoa wito kwa wananchi wa mikoa ya jirani ikiwemo Morogoro na Pwani kuja kushuhudia tamasha hili ambalo pia siku hiyo tutawaombea viongozi mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na pia tutaliombea Taifa". Alisema bw. Msama.

Aidha Bw. Msama aliongeza kuwa mpaka sasa waimbaji wakongwe wa muziki wa injili ambao wamethibitisha kushiriki ni Martha Baraka, Martha Mwaipaja na Rose Muhando ambao tayali wapo kambini kujifua kuhakikisha siku hiyo nakukonga nyoyo za wapenzi wa nyimbo za injili.

Kampuni ya Msama Promotions imekua kinara wa kuandaa matamasha mbalimbali ya Injili ikiwa ni sehemu ya kuibua na kuendeleza vipaji vya uimbaji lakini pia kuliombea Taifa na Watanzania kwa ujumla.

Tamasha la mwaka huu limepewa kauli mbiu inayosema "Tanzania ni Nchi yetu,tuipende na tuilinde" kwa lengo la  kuhamasisha na kudumisha amani, mshikamano na upendo kwa Taifa.
 

No comments