Nchi 16 Ukanda wa Afrika ya Mashariki zathibitisha kushiriki Miss East Africa 2021
Nchi 16 za Ukanda wa Afrika ya Mashariki zimethibitisha kushiriki Mashindano ya Miss East Africa 2021 yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Mashindano HAYO kwa mwaka huu, Jolly Mutesi amesema mashindano ya Miss East Africa n makubwa katika ukanda huo na kwamba yatatoa fursa ya kuitangaza nchi kiutalii pamoja na kuonyesha fursa mbalimbali za uwekezaji.
Amebainisha kuwa makampuni mbalimbali ndani ya ukanda huo yanatakiwa kutumia fursa ya mashindano hayo kutangaza biashara zao ndani na nje ya mipaka ya nchi kupitia shindano hilo.
"Mashindano haya yatakuwa endelevu yatafanyika kila mwaka yatasaidia katika kudumisha umoja wa nchi hizo, kukuza utalii, kutangaza fursa za uwekezaji hasa kwa nchi iliyoandaa," amesema Jolly.
Amesisitiza kuwa mashindano hayo yalibuniwa na Mtanzania Rena Callist na kufanyika nchini kwa mara ya kwanza mwaka 1996 kwa mafanikio makubwa na kwamba yamewahi kufanyika Burundi huku mara ya mwisho yalifanyika mwaka 2012 nchini Tanzania na kuangaliwa na mamilioni ya watu duniani kote.
Kwa upande wake Rais wa Miss East Africa Beauty Pageant ambaye pia ni Muaandaji wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya Rena Events Ltd, Callist amesema jumla ya ya zawadi zenye thamani ya Sh Mil 146 zitatolewa mwaka huu huku Mshindi wa kwanza atazawadiwa Gari jipya la kisas aina la Nissan X Trail toleo la mwaka huu lenye tamani ya Sh Mil 110.
Muuandaji huyo amefafanua kuwa mshindi wa pili wa mashindano hayo ataPATA Zawadi ya Sh Mil 11, mshindi wa tatu Sh Mil 5 na kwamba kutakuwa na zwadi nyingine kwa washiriki za thamani ya Sh Mil 20.
Aidha, amezitaja nchi zilzothibiisha kushiriki ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Ethiopia, Eriteria, Djibout, Somalia, Malawi, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Madagascar, Reunion na Mauritius.
Pia amesema washiriki wanatakiwa kuwa vigezo vikiwemo vya umri kuanzia miaka 18 hadi 26, angalau elimu ya sekondari, uwezo wa kujieleza yeye na nchi yake, urefu wa futi 5.8, mshiriki awe na tabia nzuri huku akiwafahamisha warembo wanaotaka kushiriki kujisajili kwenye mtandao wa mashindano hayo kwani watakaofuzu vigezo watafanyiwa usaili.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Matiko Mniko amesema mashindano hayo ni fursa ya nchi kutangaza vivutio vya utalii na yataagaliwa moja kwa moja na watu 300 duniani kupitia vituo vya runinga na mitandao.
Amewaomba wasichana wenye vipaji vya urembo kujitokeza kwa wingi kushiriki kwani BASATA itasimamia yale yaliyoainishwa katika mikataba pamoja na kusimamia masilahi ya washiriki wa mashindano hayo.
Na: Hussein Ndubikile
No comments