Breaking News

TMA, Wanahabari Wakutana Lujadili Msimu wa Mvua za VULI

Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dk. Ladialaus Chang’a akifafanua jambo katika semina hiyo
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombobalimbali vya habati wakisikiliza hotuba.

Kibaha, Tanzania 
BAADHI ya Waandishi wa Habari kutoka jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye semina ya siku moja leo Septemba 1.2021 katika Chuo cha Uuguzi mjini Kibaha Mkoa wa Pwani, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kuhusu mwelekeo wa utabiri wa mvua za msimu wa Vuli zitakazoanza Octoba hadi Desemba mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ufunguziwa semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a alisema kushiriki kuvijadili viashiria mbalimbali vinavyo tumika kukusanya taarifa sahihi kwaajili ya tabiri mbalimbali ikiwemo ya vuli.

Alisema Semina hiyo ni miendelezo wa semina za kila mwaka zinazoshirikisha wadau wa TMA kabla ya kutangzwa kwa utabiri wa msimu husika. Hivyo wadau hao wanapata mrejesho wa utabiri uliotangulia na mwelekeo wa utabiri ujao.

Aidha dk. Chang'a amewapongeza wanahabari kwa kuongeza wigo wa ufahamu wa taarifa za utabiri kwa jamii na kuwataka kuendelea kuandika taarifa sahihi za hali ya hewa mara kwa mara badala ya kusubiri msimu hadi msimu.

No comments