Breaking News

DCEA, Yaungana na Mamlaka za Serikali Na Sekta Binafsi Kuzuia Uchepushaji Wa Kemikali Bashirifu

Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Kusaya akifafanua jambo katika Hafla ya utiaji saini wa hati ya Makubaliano kati ya serikali na Sekta katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na Dawa Tiba. (Picha na Mtandao)

Na: Mussa Khalid
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)   kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine za serikali pamoja na sekta binafsi imetekeleza mradi wa Pamoja chini utaribu wa Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya ili kuimarisha na kuzuia Uchepushaji wa Kemikali Bashirifu na Dawa Tiba zenye Asili ya kulevya.

Akizungumza katika Hafla ya utiaji saini wa hati ya Makubaliano kati ya serikali na Sekta katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na Dawa Tiba,Kamishna Generali wa Mamlaka hiyo Gerald Kusaya amesema lengo la mradi huo ni kuweka utaratibu wa kufanya kazi kwa pamoja.

Kusaya amesema ushirikiano huo utachangia kuboresha zaidi utekelezaji wa matakwa ya sheria zilizopo kwa wadau wa serikali kuwa na jukwa na kufanya kazi na kuongeza uzoefu katika taarifa mbalimbali za udhibiti.

‘Kwa siku ya leo Mkataba huu wa makubaliano ya ushirika katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu utaanza na kampuni chache takriban 32 na vyama viwili 2 vya wadau wanaojishughulisha na dawa tiba zenye asili ya kulevya ambavyo ni TPMA na TAPI wakiwakilisha kampuni zinazofanya kazi hizo’amesema Kusaya

Afisa mauzo kutoka Taasisi binafsi ya Kemikali Charles Fubusa amesema watahakikisha wanashirikiana pamoja na Mamlaka za kiserikali ili kuendelea kupata mwongozo utakao waletea manufaa.

Churchill Katwaza ni Mwenyekiti wa taasisi TAPI inayojishughulisha na uagizaji na usambazaji wa dawa,vitendanishi pamoja na vifaa  tiba,ameahidi kuwa watashirikiana kuhakikisha udhibiti wa dawa na kemikali haziendi nje ya utaratibu uliopanga.

Katika hafla hiyo ameshiriki Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelis Mafumiko ambapo amezikumbusha Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba kuwa zina majukumu ya kusimamia kemikali bashirifu zote za viwandani na majumbani na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika matumizi yake.

No comments