NCCR- Mageuzi: Serikali Iwekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kuwapunguzia Wananchi Mzigo wa Tozo, Washanga Maagizo ya Rais Kupuuzwa
Chama cha NCCR-Mageuzi kimeishauri Serikali kuwekeza kwenye sekta ya kilmo, uvuvi na mifugo ili kuwapunguzia wananchi mizigo ya tozo zinazolalamikiwa kwenye mitandao ya simu na mafuta huku kikibainisha kuwa maagizo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan. hayatekelezwi na mamlaka husika.
Hayo yamesemwa jijijni Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Uenezi na Mahusiano wa chama hicho, Edward Simbeye wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na hali ya nchi, tozo za miamala ya simu na upandaji wa bei ya mafuta.
Alisema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa nchi zilizoelekza kikamilifu kwenye sekta hizo zimefanikiwa katika kuwahudumia wananchi wake katika huduma muhimu zikiwemo elimu, pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
"Tunaishauri Serikali kuachana na tozo zinazoumiza iwekeze kwenye kilimo, mifugo na uvuvi katika bahari kuu mzigo vikifanyika vyote hakutakuwa na tozo kandamizi kwa wananchi wake," Alisema Simbeye.
Amebainisha kuwa tozo za miamala hiyo zimepunguzwa kwa asilimia 30% na kwamba zimewekwa kwa kigezo cha kuchangia miradi ya maendeleo hivyo kwani utozaji huo ni unyang'anyi kutoka kwa wananchi kwenda kwenye mamlaka.
Amsisitiza kuwa kwenye mafuta kuna kodi 19 ambazo zingepunguzwa bei ya mafuta isingepanda hali inayochangia kupada bei ya sukari na mafuta ya kula na kwamba ulipaji ni kinyume cha utozaji kodi
Katika hatua nyingine, amesema maagizo yaliyotolewa na Rais Samia hayajatekelezwa ikiwemo Jeshi la Polisi kuacha kubambikia watu kesi na kuzifuta kesi 147, Vyam kupewa fursa ya kikatiba ya kufanya mikutano ya hadhara, jeshi hilo kucha kutumia nguvu katka kutekeleza majukumu yake pamoja kuvifungulia vyombo vya habari vilivyoofungiwa.
Aidha, chama hicho kimemuomba Mkuu wa Jeshi hilo nchini IGP Simon Sirro kuomba radhi kwa kauli yake alioitoa hivi karibuni na kujitafakari juu ya mwenendo wake kwani chuki kati ya raia na jeshi hilo inazidi kuongezeka na kwamba kuna tukio la udhalilishaji wanawake lilitoka Handeni, Tanga IGP Sirro hajalizungumzia.
No comments