Breaking News

BRELA Kutoa Huduma za Pamoja Kupitia Posta

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni miongoni mwa taasisi za Serikali zitakazotoa huduma kwa pamoja kupitia Shirika la Posta nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mapema leo huduma hizi za pamoja zinatarajia kuzinduliwa rasmi na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (Mb), Septemba, 6 2021 katika viwanja vya Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mkakati uliopo sasa ni kulifanya Shirika hilo kuwa kitovu cha Biashara Mtandao hivyo kufanya ushirikishwaji wa pamoja katika kutoa huduma kuwa ni jambo la muhimu.
Shirika la Posta litazindua rasmi huduma ambayo mbali na Taasisi ya BRELA  itazikutanisha  taasisi mbalimbali za Serikali na kutoa huduma kwa pamoja ikiwemo NIDA, NSSF, RITA, TRA, PSSSF, NHIF na nyinginezo ambazo zitatoa huduma kupitia ofisi za Posta nchini.

No comments