Breaking News

Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC) Yaja na Mwarobaini wa biashara

Katika Kuhakikisha  Sekta ya Biashara katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Uviko 19 inakuwa, Kampuni ya  World Logistics company (WLC) imezindua huduma ya mpya ya kuagiza na kusafirisha mizigo ijulikanayo Cargo Pickup Delivery Service.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Masoko wa kampuni hiyo Agnes Daniel alisema kuwa huduma hiyo inatarajia kumuhakikishia Muagizaji na Mpokeaji kuepuka usumbufu na gharama za usafiri na zinginezo.

"Huduma Hii itamsaidia anayeagiza mizigo kuepuka usumbufu nakuepuka gharama zinginezo  nakubaki Salama dhidi ya  ugonjwa wa Uviko 19". Alisema Agnes Daniel.

Bi. Agnes alisema  kupitia teknojia Muagizaji ataweza kufuatilia mzigo wake katika hatua zote za usafirishaji za mizigo kuanzia siku ya kwanza alipoagiza Mzigo na kupokea mzigo huo kwa kutumia nyenzo ya  Google Excle.
Aliongeza kuwa tofauti yao na kampuni nyinginezo za usafirishaji kampuni hiyo ambayo ina uzoefu wa zaidi ya miaka 17 imejikita zaidi kufanya shughuli zake kupitia teknojia hiyo.
Kwa upande wake Afisa Masoko wa kampuni hiyo Apaisaria Godvice alisema wafanyabiashara wamekuwa wakipata changamoto pindi wanapo agiza mzigo mfano masuala ya gharama za Kulala Hotelini, Usafiri, Kuwepo kwa masharti ya kuchanja chanjo ya Corona, kuhofia kuwekwa karantini hivyo kupitia huduma ya kuchukua mzigo popote duniani ya Cargo Pickup & Delivery Service iliyoanzishwa na kampuni hiyo itasaidia kuondoa changamoto hizo nakukuza uchumi.

"Tuna mawakala nchi nyingi duniani, hivyo tuna uhakika wa kufikisha mzigo kwa usalama, hata usafirishaji wa biashara haramu hauwezi kutokea kupitia kampuni yetu, sisi ukitupa taarifa za mzigo wako aina ya mzigo na nchi ambayo huo mzigo upo basi tunawasiliana na mawakala wetu tunahakikisha mzigo unapakiwa kama ni kwenye meli au ndege na ukifika hapa tunafanya taratibu za clearing and fowarding hadi mzigo unamfikia mteja wetu" alisisitiza Apaisaria

No comments