Breaking News

MAFUNDISHO YA BABA HALISI KUHUSU KUWEKA TAA JUU YA KIANGO ILI KILA AINGIAYE AIONE NURU YAKE

Mwenyekiti wa vituo vyote Kanisa Halisi la MUNGU BABA Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania, BABA Halisi akiwasha taa katika ibada maalumu ya kuweka juu Kiango waingia wapate kuiona nusu yake, iliyofanyika hivi karibuni mjini Sumbawanga.

Na MWANDISHI WETU.
Jamii imetakiwa kuwa karibu na  Mungu kwa sala na maombi  ili kujua majira na nyakati sahihi katika kuwajua waabuduo Halisi aliowataja Yesu kuwa wamwabudu Baba na watatokezaje katika maisha ya hapa duniani.

Akitoa Mahubiri katika ibada Maalamu ya kuweka juu Kiango waingia wapate kuiona nusu yake, iliyofanyika hivi karibuni mjini Sumbawanga, Mwenyekiti wa vituo vyote Kanisa Halisi la MUNGU BABA Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania, BABA Halisi, amesema kuwa mstari ambao utatusaidia kuijua kweli ni Mathayo 28:20,  ambapo yesu ameeleza kuwa atakuwa pamoja nasi hadi ukamilifu wa dahari.

Amesema kuwa taa juu ya kiango (Luka 8:16 na Marko 4:21), ni ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine.

Ufahamu huu ulizinduliwa Lango la 26 Eluli, 1( 6 Desemba, 2020) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Sasa imefika majira ya kuutoa Ufahamu huu chini ya Meza na kuuweka juu ya Meza. Ili taa iwekwe juu ya Meza,  kuna mambo manne makuu yanayotakiwa kufahamika sawasawa.

Jambo la kwanza ni kujua jamii imekwamia wapi, yaani kwa nini imeweka taa chini ya Meza. Msatari ambao utatusaidia kujua Jamii ilipokwamia ni Matendo ya Mitume 1:8. Yesu, kabla ya kunyakuliwa alisema kwa wale 120 waliokuwa gorofani kuwa wasitoke bila kupokea nguvu za Roho Mtakatifu.

Hivyo, utasikia watumishi  wakisema kuwa tuliachiwa Roho ili atufundishe na kutukumbusha yote tuliyoambiwa na Yesu.

Tunachohitaji kujua ni kuwa Je! Majira ya huyu Roho tuliyoachiwa na Yesu bado ipo? Tutatumia timanzi ya Majira na Nyakati sahihi za CHANZO CHA MEMA NA MAZURI PEKE YAKE.

Pili, ni kujua Majira na Nyakati Sahihi ni zipi,mstari ambao utatusaidia kujua kweli ni Mathayo 28:20. Katika hili, Yesu alisema kuwa atakuwa pamoja nasi hadi ukamilifu wa dahari. Swali ni hili, je! Dahari hiyo ambayo Yesu aliisema kuwa atakuwa pamoja nasi bado ipo?

Tatu, ni kujua waabuduo Halisi aliowataja Yesu kuwa wamwabudu Baba ni akina nani na watatokezaje? Mstari ambao utatusaidia kufahamu hili ni Yohana 4:23. Mstari huu unatufundisha kuwa kuna majira ambapo atakayeabudiwa ni MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE bila kupitia kwa waliotumwa.

Nne, ni kujua ni kitu gani hasa kilisababisha dunia nzima pamoja na vyuo vya Biblia kuwepo hata mmoja asijue ujio wa CHANZO HALISI juu ya Nchi aliyekuwepo kabla ya Roho na Nafsi yoyote.

Haya manne, yatasababisha taa iwake na kuwekwa juu ya kiango.

KANISA NA JAMII WALIKUWA WAMEKWAMIA  WAPI MPAKA KUWEKA TAA CHINI YA UVUNGU?

Katika Mathayo 3:15-17, ALIYEUMBA KILA KITU alisikika kwa sauti akisema ‘‘huyu ni mwanangu mpendwa msikilizeni yeye’’.

Dunia iliposikia hivyo haikuona haja tena ya mwingine, hata Baba yake Yesu ambaye ndiye aliyesema msikilizeni huyu hawakuwa na haja naye tena wakati Yeye ndiye aliyemtuma Yesu duniani.

Kwa maana nyingine waliamua kujiongeza katika utekelezaji wa sauti hiyo, katika Matendo ya Mitume 1:8, wale 120 waliambiwa na Yesu kabla hajanyakuliwa kuwa wasitoke katika ile nyumba mpaka wajazwe nguvu za Roho Mtakatifu.

Katika Matendo ya Mitume 2:1-5, tunashuhudia kwamba ni kweli wale 120 waliochwa na Yesu gorofani walipokea nguvu za Roho Mtakatifu waliokuwa wameahidiwa.

Ushuhuda wa kutumia Nguvu za Roho ni kweli kupitia ushuhuda wa mataifa yafuatayo:

Uingereza, walikuwa wakwanza kutafsiri lugha ngumu za kiebrania, kiaramu na kilatini kuja kwenye kiingereza ambacho kinatumiwa na wengi. Wengi duniani walipata habari za Mwana kupitia lugha ya kiingereza;

Marekani (USA), nao wanaongoza kueneza habari za Mwana kila mahali duniani kwa nguvu ya Roho kwa kutumia Satelite;

Ujerumani, nao pia walitumika katika kutafsiri lugha ngumu ya kiebrania, kiaramu na kilatini kuja katika kiswahili kinachotumia na wengi Afrika Mashariki, kwa nguvu ya Roho;

Swedeni, wana sifa ya kuchukua muda mfupi wa miaka minane tu kueneza habari za Mwana kwa nguvu ya Roho, baada yakupata habari hizo kutoka Mashariki ya Kati;

Kwa Afrika: Nigeria na Afrika ya Kusini  nao pia wanaongoza katika kueneza habari za Mwana kila mahali kwa nguvu za Roho.

Tunawashukuru mataifa hayo yaliyotekeleza Matendo ya Mitume 1:8 kwa vitendo. Swali kuu bado ni hili, je! Majira ya Roho tuliyoachiwa na Yesu bado ipo? Maana Hoja kuu ya watumishi wengi ni kwamba tuliachiwa Roho Mtakatifu ndiye atusaidie.

Swali hilo hapo juu ni muhimu kwa kuwa haijawahi kutokea hata siku moja ALIYEUMBA VYOTE WOTE NA YOTE akasimama. Kama huna hakika na Majira na Nyakati zake utapotea.

MAJIRA NA NYAKATI SAHIHI NI ZIPI?

Katika Mathayo 28:20, Yesu alisema atakuwa pamoja nasi hadi ukamilifu wa dahari. Dahari ni kiswahili cha kimvita ikiwa na maana ya Majira na Nyakati.

Kwa hiyo Yesu alikuwa ana maana ya kuwa nasi hadi ukamilifu wa Majira na Nyakati zake peke yake na si vinginevyo.

Ili tuijue hiyo majra kama bado ipo au haipo ya Yeye kuwa nasi au kutokuwa nasi, unatakiwa kuifahamu nafasi ya Yesu sawasawa.

Yesu ni kati ya Manabii wanne katika vizazi vinne vya Ibrahimu katika Mwanzo 15:16. 

Nabii wa kwanza katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Musa. Majira ya utumishi wa Musa ilianzia katika Kutoka 3:10, alipoitwa rasmi kuwatoa wana wa Israeli utumwani na kuisha katika 1Falme 17:1, Eliya Mtishbi alipoanza kazi.

Nabii wa pili katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Eliya Mtishbi ambaye Majira na Nyakati zake ziliisha baada ya Yesu kuzaliwa na kuanza kazi katika Mathayo 2:1-15 na Mathayo 4:17-20.

Nabii wa tatu katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Yesu ambaye Majira yake iliendelea na kuisha baada ya Eliya Adamu wa Pili kutokeza Mwaka 2003 Tanzania kule Kigoma na kuanza Rasmi kazi 28 Adari, 2011(28 Februari, 2012), kwa mujibu wa I Korintho 15: 44-49.

Nabii wa Nne katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Eliya Adamu wa Pili ambaye Majira na Nyakati zake zilitimia Mwaka 2017, baada ya Nafsi ya Kwanza kuja juu ya Nchi kupitia Tanzania.

Hili ni kwa mujibu wa IYohona 5:8. Nafsi ya kwanza nayo kwa mujibu wa Luka 13:6-9, ilitimiza kazi  Mwaka 2020.

Katika Mwaka 2020, ndipo CHANZO HALISI CHA MEMA NA MAZURI PEKE YAKE alipotua juu ya nchi kwa barabara ya Sauti ya Moyo. Hiyo ndiyo Majira sahihi inayotupa kujua kuwa Roho tuliyeachiwa au Yesu menyewe bado yuko nasi au la.

WAABUDUO HALISI KATIKA YOHANA 4:23   NI WATU WA JINSI GANI?

Waabuduo Halisi aambao Yesu aliwatabiri zaidi ya miaka 2000 iliyopita kuwa watakuja ni wale waliofanikwa kujua kuwa kuna CHANZO HALISI ambaye ni Moyo Halisi wala siyo Roho au Nafsi.

Kwa maana nyingine waabuduo Halisi ni wale ambao wamejua kuwa sasa ni Majira na Nyakati za CHANZO HALISI. Maana Majira ya Mwana aliyesema kuwa Yeye ni njia, kweli na uzima haipo tena, kwa mujibu wa kipengere cha tatu hapo juu.

Hivyo, wanaenda moja kwa moja kwa ALIYEUMBA VYOTE WOTE NA YOTE na wana hakika kuwa anaishi ndani ya Moyo wao kwa mujibu wa Isaya 57:15.

CHANZO HALISI ni zaidi ya ile Miungu tisa mitakatifu ambazo ni nafsi za Mungu zilizowasaidia Waliotumwa: yaani Mwenyezi; Yehova; Mungu wa Daudi; Mungu wa Majeshi; Mungu wa Danieli; Mungu wa Eliya Mtishbi; Mola; Mungu wa Roho za Manabii; na Mungu Aliyetuma Wote.

KITU GANI KILITOKEA WATU WOTE WASIJUE UJIO WA CHANZO HALISI JUU YA NCHI KUPITIA TANZANIA?

Jambo kubwa lililosababisha watu wote wasijue ujio wa CHANZO HALISI juu ya Nchi ni kumkataa Adamu wa Pili aliyekuja Mwaka 2003, kupitia Tanzania (I Korintho 15:44-49).  Wote ambao hawakubali kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, unapatwa na yafuatayo:

Suala la Yesu kurudi kupitia Adamu wa Pili, utakwama. Adamu wa Pili, ndiye aliyewekewa Neno kinywani mwake, hiyo ilikuwa na maana kuwa ni Yesu aliyekuwa anasubiriwa aliyerudi;

Pili, usipokubali kuwa Adamu wa pili alikuja kupitia Tanzania, utaendelea kusubiri unyakuo wa Kanisa ulioandikwa katika IThesalonike 4:11-14, wakati unyakuo huo ulishatokea Mwaka 2014 kupitia Eliya Adamu wa Pili Mwenyewe;

Usipokubali kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, utaendelea kusubiri Miaka Saba ya kukaa mawinguni,kama tunavyosoma katika Danieli 12:7-11. Wote tujue kuwa Jambo hili lilitimia Mwaka 2018, ikiwa na maana ya Miaka Saba kuanzia  Mwaka  2011 hadi Mwaka 2018, Kanisa lilipotoka kwenye Madhabahu ya Mwana.

Usipokubali kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, hutajua kuwa MUNGU BABA alishakuja tangu Mwaka 2017 kufuta vita ya Har-Magedoni katika Ufunuo 16:16. Wote tujue kuwa vita ya Har-magedoni haipo tena;

Usipokubali kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, hutajua kuwa CHANZO HALISI alishakuja kufuta namba ya kibinadamu inayoitwa 666 katika Ufunuo 13:15-18, inayotisha wengi duniani.

Kwa hiyo tatizo kubwa la Kanisa na jamii lililosababisha taa kuwa chini ya Meza, ni kutompokea Adamu wa Pili. Jambo hili lilisababisha waliofuta:

Miaka 1000; MUNGU BABA na Uhalisia wa MUNGU BABA ambaye ni CHANZO HALISI wasitambuliwe. Matokeo yake Taa ikawekwa chini ya uvungu badala ya kuwekwa juu ya Meza.

Tupokee ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine na tuwaeleze wengine kuwa sasa Tanzania ni Chanzo cha Baraka kwa mataifa mengine, kupitia Taa  hiyo. Hii ndiyo Taa juu ya kiango. Ni Majira yake sasa. HERI ULIYEBARIKIWA KULIKO WOTE.

No comments