LHRC: Matukio ya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Yaongezeka Nchini
Na:Timoth Marko, Dar es salaam.
Kituo cha haki na Binadam nchini kimesema kuwa Hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto umeongezeka kutoka 23,685 Kwa Mwaka 2019 Hadi kufikia matukio 36,940 Kwa Mwaka 2020 .
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kituo hicho Anna Henga alisema ongezeko hilo nisawa na Asilimia 5.7 ambapo katika matukio yaliyo ripotiwa katika Vituo vya polisi ni 36,940 ikilinganishwa na matukio 7,388 Kwa Mwaka.
Katika hatika hatua nyingine Kituo hicho, kimeanzisha mbio Maalum zijulikanazo haki marathon zinazolenga kutafakarisha umma wa watanzania juu ya kuheshimu haki za binadamu ambapo kilele chake ni Desemba 10 Mwaka huu.
Anna Henga alisema wazo la Kufanya mbio hizo Kwa njia ya Mitandao ni mkakati wa kituo hicho kujenga uelewa na kuwawezesha watanzania kutambua wajibu wao wakulinda haki za binadamu nchini.
"Janga hili linaloendelea la Uviko 19 limeilazimisha kituo cha sheria kwa njia ya Mitandao ili kuzingatia miongozo ya afya". Aliongeza Henga.
Kwa upande wake Mratibu wa Haki Marathon Deus Ntukamazima amesema mkimbiaji katika mbio hizo atatakiwa kujisajili moja kwa moja katika tovuti ya Haki marathon .
Amesema mkimbiaji atapaswa kuwa na simu janja ambayo kwani baada ya kumaliza kukimbia tovuti ya Haki marathon itaweza kuoenesha ni kwa kiasi gani amekimbia.
No comments