Breaking News

Mshindi Miss Tanzania Eastern Zone 2021 Kuondoka na Kitita cha Mil 2

Shindano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo kanda ya Mashariki lijulikanalo kama Miss Tanzania Eastern  Zone linatarajiwa lifanyika septemba 24  mkoani Morogoro.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kampuni ya Tips Forum, Mhandisi Nancy Matta alisema maandalizi yote yamekamilika na kubainisha kuwa mshindi atawakilisha katika mashindano ya kitaifa ya Miss Tanzania.

"Mwaka huu shindano litaanzia ngazi za mikoa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro ambapo washindi 16 watakao patikana watashiriki katika fainali ngazi ya kanda ya Mashariki" Alisema Mhandisi Nancy
Alisema mwaka huu wamejipanga vizuri zaidi kuhakikisha shindano hilo linakuwa la kipekee zaidi ili kupata mshindi ambae anaweza kunyakua taji la Miss Tanzania na kuiwakilisha nchi vizuri

"Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika katika hoteli ya Morena ambapo mshindi wa kwanza atapata kitita cha shilingi milioni 2, mshindi wa pili sh milioni 1.5  na mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha sh milioni 1"

Aidha Mhandisi Nancy aliongeza kuwa lengo kubwa la shindano halo ni ukiachana na kukuza sekta ya urembo ni kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake moja ya wadhamini wa mashindano hilo Bodi ya Taifa ya utaliii (TTB), BI Maria Mafie alisema wameamua kudhamini mashindano  hayo ya ulimbwende ili kuweza kukuza na kutangaza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.

Nae afisa masoko hoteli ya Dynasty Beach ambayo washiriki wa kinyanganyiro hicho wameweka kambi Bw. Charles alisema wataendelea kuunga mkono mashindano hayo na ana imani mshindi ataweza pia kuibuka na taji katika mashindano ya Miss Tanzania.

Kwa upande wake Meneja mauzo wa hoteli ya Serena Bw. Shaban  Kaluse alisema kuwa wameamua kuwa sehemu ya wadhini wa mashindano hayo wakiamini kuwa yatakuwa chachu ya kuutangaza utalii wa Tanzania.

Miss Tanzania Eastern  Zone ldhaminiwa na makampuni mbali mbali ambapo mdhamini mkuu mwaka huu ni chanel ya Utalii ya  Taifa (Tanzania Safari Channel) ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC).

No comments