Breaking News

Kituo Cha Matibabu Kwa Kutumia Nyuki na Mazao Yake Chazinduliwa Jijini Dar es Salaam

Kampuni ya Tanzania International Bee imezindua kituo cha matibabu kwa kutumia nyuki na mazao yake ili kuweza kutoa huduma za afya kwa watanzania.

Uzinduzi huo umefanyika  Ubungo jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo imekua ikijihusisha na uchakataji wa mazao ya nyuki ambayo pii imekuwa ikikuza sekta ya ajira kwa watanzania.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Mgeni Katibu tawala wa Halmashauri ya Walaya ya Ubungo James Mkumbo alisema hatua hiyo imesaidia kutoa huduma bora za matibabu kwa kutumia nyuki na mazao yake nakwamba serikali wilayani humo itaendelea kuiunga mkono taasisi hoyo katika kutatua changamoto mbalimbali inazokumbana nazo.

Alisema sekta ya afya siyo biashara bali ni huduma, ndio maana serikali inasisitiza kuzingatia lishe bora, kufanya mazoezi, hivyo mtu yeyote anayefanya jambo zuri la kupunguza msongamano wa watu kwenda hospitalini ni jambo zuri na linapaswa kuungwa mkono, hivyo sisi kama serikali tunaiunga mkono taasisi hii" alisema.

Serikali ipo na nyinyi bega kwa bega popote mtakapopata changamoto tutasaidiana kuzitatua, lakini pia nawaomba mhakikishe kampuni yenu ina uhakika wa bidhaa na ubora kwa kushirikiana na wadau wengine ili kujiimalisha katika anga za kimataifa na kuwezesha sekta ya ufugaji nyuki kufanyika kibiashara" amesisitiza Mkumbo.

Awali Mtaalamu wa Matibabu kwa kutumia Nyuki na Mazao yake Dkt. Musiba Poul  alisema kampuni hiyo imekua ikikumbwa na changamo mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa elimu kuhusu matibabu ya nyuki pamoja na kuwepo kwa upungufu wa mazao ya nyuki.
Aidha Dr. Musiba ameiomba serikali iwawezeshe vijana wa wilaya ya ubungo waweze kufanya shughuli ya ufugaji wa nyuki kwani sekta hiyo bado inaonekana ni changa kutokana na vijana wengi kutokutambua kua mazao ya nyuki ikiwemo maziwa, Nta yamekuwa na soko kubwa.

"Kampuni yetu inampango wa kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya nyuki ili kuyaongeza thamani, hivyo tunaomba vijana na makundi mbalimbali yawezeshwe ili yaweze kufanya biashara ya ufugaji wa nyuki kwani mazao yake yana thamani kubwa" alisema Dr. Musiba.
 

No comments