Waziri Ummy Awapa Siku 5 Wakurugenzi Walio Teuliwa Kuripoti Kazini
Waziri Wa Nchi Ofisi Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka Wakurugenzi wote walio teuliwa kuripoti Vituo walivyo pangiwa ndani ya siku tano kuanzia Agost 3 mwaka huu kupitia kwa Makatibu tawala wa Mkoa
Agizo hilo amelitoa Jijini Dar es saalam wakati akitoa taarifa ya awali kuhusu uteuzi wa wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji, na wilaya walioteuliwa na Rais mhe. Samia Suluhu agosti moja mwaka huu.
Sanjari na hayo alisema Wakurugenzi Wawili ambao majina yao yameonekana kutokea kwenye maeneo zaidi ya moja wataripoti kwenye kituo ambacho jina limeonekana kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya uteuzi.
Aidha uchambuzi wa awali ulifanywa na tamisemi wakurunzi 45 wameendelea kuwepo kwenye vituo vyao vya kazi, 70 wamehamishwa, 69 ni wapya, 15 wamejaza nafasi zilizoachwa wazi huku 54 kuchus nafasi za wakurugenzi ambao uteuzi wao umetrnguliwa.
Kadhalika kati ya wakurugenzi wapya 69 wanawake ni 33 sawa na asilimia 48 na kufanya idadi ya wakurugenzi wanawake kuws 55 sawa na asilimia 29 ya wskurugenzi wote wa mamlaka za serikali za mitaa.
Post Comment
No comments