Watetezi wa Haki za Binadamu Wakutana Jijini Dar
Katika kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu wanalindwa, Tume ya haki za binadamu na Asasi za kiraia wamekutana katika kikao kazi chenye lengo la kuwajengea wezo watetezi wa haki za binadamu nchini.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Bw. Mohamed Hamad alisema lengo kubwa la kikao ni kuwajengea uwezo Watetezi wa Haki za Binadamu kufatia Azimio la markrbisho ya sheria ambayo inaitaka serikali na Asasi za kiraia kuwalinda watetezi wa Haki za Binadamu.
"Jukumu la kuwalinda Watetezi wa Haki za Binadamu ni la watu wote ikiwemo Asasi za Kiraia, Polisi pamoja na Serikali" Alisema Bw. Hamad.
Alisema swala la kutendewa haki ni swala la kisheria hivyo kila mtu anatakiwa kutendewa na kupatiwa haki.
Bw Hamad aliongeza kuwa mtu yeyote ambaye ajatendewa haki katika mkono wa waa sheria Tume inayo mamlaka ya kisheria kuingilia kati.
"Haki za binadamu mtu apewi mezani bali anapewa mahakamani"
Nae mwenyekiti wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Bw. Onesmo Ole Ngurungwa alisema wadau wa Haki za Binadamu wanao mchango mkubwa kayika kuhimiza haki za binadamu.
Alisema kikao hicho ni muhimu kwa watetezi wa haki za binadamu kwa kuhakikisha sheria zinafatwa.
" Swala la Haki za Binadumu sio suala la fasheni ni suala la kibinadamu"Alisema Ole Ngurungwa.
No comments